KAMPUNI ya Scania nchini Tanzania imekutanisha wadau mbalimbali
wakiwemo wafanya biashara wa mabasi ya abiria pamoja na wafanya
biashaya ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya abiri kutoka makampuni
mbalimbali wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Chesisi za Scania
yaliyoandaliwa na Kampuni ya Scania yaliyojulikana kama “ Scania Bus
Expo” yaliyo fanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi
yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mauzo wa Kampuni ya
Scania Tanzania, Godwin Rwegasira alisema leo ni siku ya
kuwakumbusha wafanya biashara wa mabasi ya abiria na watengeneza
mabodi kuwa watumie Chesisi za Scania kwa wale ambao hawajawahi
na wale ambao wanatumia waendelee kutumia kwani ni bora,imara na
zinadumu kwa muda mrefu na zaidi ya yote spea zake zinapatika mahali
pote kwenye vituo vya Scania.
Alisema Rwegasira, Scania ni vumilivu sana inaweza kuhimili
miundombini ya namna yeyote hususani barabara zetu za Afrika
mashariki za vumbi, hivyo tutumie chesisi za Scania mkombozi kwa
biashara yako ya mabasi ya abiria.
Nae Afisa mauzo kutoka Kampuni za kutengeneza mabodi ya mabasi ya
Master kwa niaba ya watengeneza mabodi kutoka makampuni
mbalimbali alisema Chesisi za Scania ni bora, zina zinahimili shida, ni
imara na spea zake zinapatikana hivyo kwa niaba ya watengeneza
mabodi alitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia Chesisi za Scania
katika biashara zao za mabasi ya abairia.
Makampuni mabalimbali ndani nan je ya nchi yalialikwa katika
maonyesho hayo ambayo ni Master Fabricator kutoka Kenya, Dar Coch
kutoka Tanzania, Choda kutoka Kenya, LSHS kutoka Tanzania, Quality
Garage kutoka Tanzania, Stanbic Bank na Scania Finance pamoja na
wafanyabishara wa mabasi ya abiria.
Meneja Mauzo na masoko wa kampuni ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya abiria ya Choda kutoka Kenya, Pius Wambua(kulia) akiwaonyesha wageni waalikwa baadhi mabasi waliyowahi kutengenezwa na kampuni hiyo katika picha wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Scania yaliyojulikana kama “Scania Bus Expo” yenye malengo ya kuhamasisha wafanyabiashara wa mabasi ya abiria kutumia Chesisi za Scaina.Maonyesho yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendao mikoani cha Ubungo Dar es Salaam.
Meneja mauzo wa Kampuni ya Scania Tanzania, Godwin Rwegasira(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Chesisi za Scania yaliyojulikana kwa “Scania Bus Expo” yenye malengo la kuwahamasisha wafanya biashara wa mabasi ya abaria kutumia chesisi za Scania kutokana na ubora wake.Maonyesho hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni watengeneza mabodi wa mabasi ya Abiria, Pius Wambua meneja mauzo na masoko kutoka kampuni ya Choda Kenya(kushoto) na Peter Gitau Afisa mauzo ktoka kampuni ya Masters kutoka Kenya.
Afisa masoko wa kampuni ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya, Master kutoka Kenya, Peter Gitau(kushoto) akiwaonyesha wageni waalikwa baadhi mabasi waliyowahi kutengenezwa na kampuni hiyo katika picha wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Scania yaliyojulikana kwa “Scania Bus Expo” yenye malengo ya kuhamasisha wafanyabiashara wa mabasi ya abiria kutumia Chesisi za Scaina.Maonyesho yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendao mikoani cha Ubungo Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...