Uongozi wa Tanzania Fellowship Churches
unatarajia kufanya mkesha
mkubwa kitaifa wa kuliombea Taifa,Desemba 31 katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Mkesha huo una lengo la kuliweka Taifa mbele ya usalama wa
Mungu pamoja na kupatikana amani na
utulivu kwa Taifa zima kwa ujumla.
Akithibitisha kuwepo kwa
mkesha huo kitaifa,Mwenyekiti wa mkesha huo kitaifa,Mchungaji Geodfrey
Mallasy amesema mkesha huo una
lengo la kuliombea Taifa
na kupatikana amani na utulivu.
“Mkesha huu una lengo la kuliweka Taifa letu mbele ya usalama wa Mungu na kuliombea Taifa letu amani
na utulivu kutokana na bila amani hakuna kinachowezekana”alisema Mallasy.
Aidha,Mallasy ameeleza kuwa mkesha huo utahudhuliwa na mgeni rasmi ambaye ni Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohammed Gharib Bilal badala ya Rais Jakaya Kikwete
kuomba radhi kutokana na tatizo la kiafya.
Hata hivyo,uongozi wa
Tanzania Fellowship umeandaa usafiri kwa kampuni ya mabasi ya UDA kutoa huduma
ya usafiri siku ya mkesha,pamoja na kutengeneza
timu moja ya waimbaji,kukusanya sadaka zikazosaidia kuandaa mkesha mwingine utakaokuja
Nchi yetu inahitaji maombi
ReplyDeleteNadhani nia ingekua kuliombea Taifa tusipate njaa, tuwe na mvua za kutosha, maradhi yaondoke,watanzania wasome kwa bidii katiba pendekezwa mambo mengine yatapatikana kwa box la kura tu hayaombwi ktk viwanja......
ReplyDeleteKuwakumbusha watu wafate kanuni za maadili na serikali pia.
ReplyDelete1. wasile rushwa
2. serikali ilipe mshahra wa kikidhi ugumu wa maisha
3. wasipendelee kwa misingi ya (kabila, dini, rangi, mahali, nk.
4...
tulishabarikiwa saana.
sisi wajibu wetu ni kufuata maadili kwani tunataka Mungu ndo atufanye wanamaadili? Ye atasema ametupa utashi (free will) ili tuchague baraka au adhabu kwa kuchagua kitendo muafaka.