Mkurugenzi wa Mahusiano ya kimaendeleo wa Klabu ya Arsenal Bw. Sam Stone
(Kulia) akimkabidhi jezi ya timu hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF Bw. Adam Mayingu. Kushoto ni Bw. Daniel Willey, Meneja wa Mahusiano ya
Kimaendeleo ya Arsenal. Maafisa hao wapo nchini kwa lengo la kukutana na wadau
mbalimbali ili kufungua mahusiano ya kibiashara, katika mpango huo makocha wa
timu hiyo na baadhi ya nyota waliowahi kuchezea timu hiyo watapata fursa
kutembelea Tanzania. Klabu ya Arsenal ni kati ya klabu maarufu ulimwenguni
ambayo inashiriki ligi maarufu duniani ya Barclyas.
Mkurgenzu Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu (kushoto) akimkabidhi zawadi Afisa
Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Bw Imani Kajura ambaye ni mwenyeji wa maafisa
kutoka klabu ya Arsenal ambao wapo nchini kwa ajili ya kukutana na wadau
mbalimbali kwa lengo kufungua mahusiano ya kibiashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...