Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, George Shumbusho, akikata utepe kutambulisha kadi ya “Faida EMV Debit Card” itakayochukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki ya Exim, David Lusala (kulia) na Afisa masoko wa benki hiyo, Noel Tuga.  Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
 Mkuu wa kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki ya Exim, David Lusala (kulia),akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutambulisha kadi ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Kushoto ni Mkuu wa Hazina wa benki hiyo, George Shumbusho. Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, George Shumbusho (kushoto), akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutambulisha kadi ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki hiyo, David Lusala. Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
 
Katika jitihada za kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa wateja wake katika mazingira salama zaidia Benki ya Exim imetambulisha kadi mpya ya kimataifa ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” zilizokua zikitumika hapo awali.

Kadi hiyo mpya hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja ikiwa na mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika. Hii itasaidia wateja wa benki hiyo kutekeleza miamala yao katika mfumo ulio salama zaidi.  

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana,  Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho alisema kadi hiyo mpya ina usalama ulioimarishwa zaidi kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ na kufanyika kwa ukaguzi wa ziada wa namba ya siri.

“Tunatambua hitaji la wateja wetu kuweza kufanya miamala yao kwa usalama zaidi. Kwa kutumia kadi hii mpya ya kimataifa kutoka Benki ya Exim, mteja anaweza kuwa na uhakika kwamba miamala yake inafanyika katika mazingira salama kabisa,” alisema Bw. Shumbusho.

Aliongeza kuwa, Kadi hiyo mpya ya kimataifa inamuwezesha mteja kufanya miamala duniani kote katika mashine za ATM na POS zilizothibitishwa na MasterCard.

“Kama Benki ya Exim, tunaamini kuwa ugunduzi ni maisha. Hivyo basi, tutaendelea kugundua teknolojia mpya zitakazoendana na kasi ya ukuaji wa utandawazi katika dunia hii ya sasa ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika usalama wa kimtandao.

“Ni matumaini yetu kuwa wateja wetu watazifurahia zaidi kadi zao mpya za “Faida EMV Debit card,” alisema. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. tunashukuru kwa kujidhatiti na usalama hela za wateja ila gharama yake kwa mwaka ni kubwa sana kwa sisi wateja wakawaida, salio linapunguzwa bila makubaliano.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...