Umoja wa klabu za michezo za maveterani Dar es salaam, chini ya uratibu wa klabu za Singasinga na Tazara, unatangaza rasmi kwamba shughuli ya kurehemu wanachama wenzetu ambao wametangulia mbele ya haki itafanyika JUMATATU 12/1/2015, ikiwa pia ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi.
Ratiba itaanza Saa 7 mchana katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es salaam. Dua zitafanyika kutoka kwa Father Oscar na Sheikh Kipoozeo. Dua hizo zitafuatiwa na Chakula cha pamoja cha mchana kitachoandaliwa na Mpishi maarufu nchini, Chef Saidi Bajia, na baadae burudani mbalimbali za nguvu zitaendelea.
Karibuni tujumuike wote...
Pichani chini ni shughuli kama hii zilizofanyika miaka iliyopita.
- Imetolewa na Balozi Cisco Mtiro, Mratibu mkuu wa shughuli hii.
wanachama wa klabu za michezo za maveterani Dar es salaam wakiwa katika shughuli hiyo ya kuwakumbuka wenzao miaka ya nyuma
Mapochopocho
wadau
Kila mtoto wa mujini alikuwepo
Vilaji
Thanks very much Ambassador Cisco. Great important event. Please do list the names as much as you can. Last time I went through the list, I had a shock of my life to hear Saad S of TAZARA passed away.
ReplyDeleteAhsante and thanks for organising this again and all the best.
Mdau - Australasia
muombeni miola wetu mlezi awarehemu wote waliotangulia halafu kuleni chakula mkimaliza mtawanyike msianze kupiga mambo yetu yale (mvinyo)
ReplyDelete