Na Bashir Yakub
Mara nyingi nimekuwa nikiandika kuhusu masuala muhimu kuhusu ardhi hasa namna ya kuandika mikataba mtu anapokuwa ananunua nyumba/kiwanja , hadhi ya mikataba hiyo kisheria, na ubora wake.
Pia nimeandika mambo mbalmbali kuhusu namna ya kununua nyumba au kiwanja kwa usalama ili watu wasitapeliwe. Nikasema suala si tu kununua kile unachokipenda na kuondoka isipokuwa ni kununua na kuwa salama na ulichonunua bila hatari ya kukumbana na mgogoro mbeleni.
Lengo la haya yote ni katika kuhakikisha watu hawatapeliwi na hivyo kupoteza fedha walizochuma kwa jasho.Lengo lingine ni kuwaepusha wanunuzi na hatari ya kuingia mahakamani ambako kuna usumbufu mkubwa na panapoteza fedha na muda sana tena sana, naongea hili kwa uzoefu.
Leo pia nasisitiza tena kuwa ili ununue kiwanja au nyumba na uepuke kabisa kupata mgogoro hakikisha unafuata taratibu zote za msingi na za kisheria ikiwemo kuhakikisha unaandaa mkataba wenye hadhi ambao hata likitokea tatizo basi mkataba uwe ndio mlinzi wako. Aidha leo naongelea tatizo lingine tena katika masuala hayahaya ya manunuzi ya viwanja na nyumba. Naongelea fedha ambayo serikali za mitaa wamekuwa wakiichukua kutoka kwa watu wanaouziana ardhi.
Dah ahsante kwa kunijuza...Me nilikuwa sijui kuwa haiko katika sheria !! Dahhh walinisumbua sana hawa....Ngooja now nimeshafumbua macho
ReplyDeleteWewe mwanasheria, usije ukatuingiza mkenge, tukanunua nyumba, viwanja, halafu vikawa na migogoro, aidhi vimeuzwa mara kumi, halafu wewe unasema sio lazima kupitia serikali za mitaa, wakati serikali za mitaa ndio wahusika/wenyeji wa maeneo hayo. hebu tueleweshe vizuri mwanasheria. mimi nilikwenda kununua kiwanja yombo vituka, kumbe huyo mwenye kiwanja alikuwa tapeli, kilichoniokoa ni serikali za mitaa, na nikawa nimeokoa pesa yangu. sasa kama kweli sharia ndivyo inavyosema, nina mashaka kidogo. pia juzi nilinunua shamba hekali kumi, bila kupitia serikali ya mitaa, kumbe wauzaji walikuwa ni walinzi wa eneo hilo, na mara baada ya muda tukakamatwa kama wavamizi wa shamba hilo. kwa kweli ingekuwa tumepitia kwenye serikali ya mtaa tusingepata shida hiyo. hapo unasemaje?
ReplyDeletemwanasheria asante sana klwa hili na asante kwa kutujuza kaka
ReplyDeleteAsante sana kwa kuelimisha umma katika masswala ya ununuzi na uuzaji wa ardhi na nyumba. Watanzania tunahitaji elimu, na elimu tu ndio itatukomboa. Inasikitisha sana kuona kwamba rushwa imekuwa kama ni kiungo cha muundo wa serikali ya Tanzania.
ReplyDeleteje ? ukitaka ku repair nyumba,kama kubadilisha bati au ukuta umeanguka ni lazima kuomba kibari serikali za mitaa au kuwausisha
ReplyDelete