Ofisa Kumbukumbu wa Benki ya NBC, Telesfori Gabriel (wa tatu kushoto) akibonyeza kitufe cha kompyuta ili kupata mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Mkazi wa Bukoba, Josephat Gerald Ruyongo ameibuka kidedea wa zawadi ya gari jipya aina ya Nissan Double Cabin Pick Up 2014 yenye thamani ya zaidi ya shs milioni 54.Wengine kutoka kushoto Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao, Meneja katika Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa cha Benki ya NBC, Dorothea Mabonye na Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia) akizungumza wakati wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Pamoja naye ni Meneja katika Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa cha Benki ya NBC, Dorothea Mabonye.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya NBC, Irene Peter (kulia) akizungumza na mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Mkazi wa Bukoba, Josephat Gerald Ruyongo ameibuka kidedea wa zawadi ya gari jipya aina ya Nissan Double Cabin Pick Up 2014 yenye thamani ya zaidi ya shs milioni 54.Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao na Meneja katika Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa cha Benki ya NBC, Dorothea Mabonye.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...