HATIMAYE
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama,
ameibuka na kutamka yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose
Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo
kwa waimbaji wengine.
Kwa mujibu
wa taarifa ya Msama kwa vyombo vya habari jana, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote
wa muziki wa Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokana
na nafasi yake
katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15.
Msama, mtu
aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na
kuandaa matukio ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na
Tamasha la Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu
ambayo amekuwa akipata juu ya Rose.
“Nimekuwa
nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji,
kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayomualika na
kushindwa kutokea.
“Lakini, naomba
watumishi wa Mungu wanielewe katika hili, sipokei mialiko wala simzuii Rose. Mimi
ninapokuwa na matamasha, nimekuwa nikimualika kama
wafanyavyo wengine.
“Nimekuwa
nikimlipa kiasi cha fedha anachotaka na hakuna zaidi, hivyo mimi sio Meneja
wake,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza:
“Agosti
mwaka huu, kampuni yangu ilidhamini uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la
Yesu, haikuwa na maana kwamba ni Meneja wake.
“Nilimualika
uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu Oktoba mwaka huu, nilimlipa
fedha, lakini hakutokea kama ambavyo amekuwa
akifanya kwa wengine ambao wamekuwa wakilalamikia tabia hiyo,” alisema Msama.
“Pia wiki
iliyopita nilikuwa na Tamasha la Krismasi tulikubaliana aje katika maonesho hayo,
lakini hakutokea na tulishamlipa,” alisema Msama kwa masikitiko na kuongeza
kuwa amemsamehe na anamuombea kwa Mungu aweze kubadilika.
Alieleza
kuwa hana tatizo na mwimbaji huyo, wala hana ugomvi naye, lakini amekuwa
akipata taabu kutoka kwa baadhi ya wachungaji pale Rose anapoalikwa halafu
hatokei na inaonekana yeye ndiye amemzuia.
“Sijawahi
kupokea mialiko kwa niaba ya Rose, kila kitu anafanya mwenyewe, hivyo ni vyema
wadau wakafahamu hilo,”
alisema Msama na kusema angekuwa mwepesi wa kulalamika, angeshafanya hivyo muda
mrefu dhidi ya Rose.
Aidha, Msama
amekana kuhusiana na madai ya Rose kutumia dawa za kulevya na kusisitiza kuwa
hajawahi kumuona akijidunga kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa
vikiripoti na kuongeza kama ikiwa ni kweli, hilo pia ni suala binafsi.
“Baadhi ya
vyombo vya habari vinaandika ni mjamzito, nafikiri pia hayo ni mambo yake
binafsi na hakuna mtu mwenye haki au uhalali wa kuhoji hilo.Yule ni mtu mzima
na mwenye kujielewa,” alisema Msama.
Rose ni
mwimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini aliyejipatia sifa ndani na nje ya
ukanda wa Afrika Mashariki ambaye mwishoni mwa mwaka 2013, alisaini mkatabawa kufanya
kazi na kampuni ya muziki ya Sony ya Afrika Kusini.
Miongoni mwa
albamu zilizompa umaarufu Rose kiasi cha kuwa alama ya mafanikio ya muziki wa
injili nchini, ni ‘Uwe Macho,’ Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange
Sawasawa, Kitimutimu, ‘Mungu Anacheka’ na Wololo na Kamata Pindo la Yesu aliyoachia
hivyo karibuni.
ETI MLEZI WA WAIMBAJI WOTE WA NYIMBO ZA INJILI!!!
ReplyDeleteKWA MAMLAKA YA NANI? Anawajua waimbaji wote wa nyimbo za injili huyu Jamal???
Watu wengine bwana.
Mwambie anajipachika vyeo hasivyokuwa na sifa navyo hadi aibu, eti huwa namlipa hela anayotaka,
ReplyDelete