Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita Ndugu.Josephat Msukuma akizungumza na wananchi wa Morogoro Mjini wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara akiwasalimia wananchi wa Morogoro Mjini hii leo.
Comrade Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Morogoro Mjini,Mwigulu amesisitiza wananchi kusimamia Vizuri Mali za Umma hasa kwa Viongozi waliopewa dhamana,Pia amesisitiza wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la kupiga kura.
Mkutano Ukiendelea Morogoro Mjini.

Mwigulu Nchemba amehitimisha ziara yake ya Kutembelea Mkoa wa Morogoro wote hii leo kwa Kufanya Mkutano Mkubwa Morogoro Mjini.
Katika ziara yake Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu katibu Mkuu CCM Bara amesisitiza Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura,Amesisitiza Viongozi waliochaguliwa serikali za Mitaa kutumia dhamana waliyopewa kwa Maslahi ya Watanzania wote,Pia amesisitiza kuwa hakuna nafasi ya Kulea wezi wa Mali ya Umma,CCM hainamkataba na wezi wa mali ya Umma.Mtu anayeiba Fedha za umma,Mtu anayeiba Madawa Hospitalini,Mtu anayetumia madaraka yake Ovyo ni Mtu asiyevumilika,hastahili kujiuzuru tu,Ni lazima hatua za Kimahakama zifuatwe na afilisiwe.

Mwisho,Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa CCM imetekeleza Ilani yake vizuri sana na bado wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo,hivyo Watanzania waendelee kuwa na Imani na chama cha Mapinduzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...