Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla amefanya ziara ya vijiji mbalimbali Mbeya Vijijini ambako amezindua mradi mkubwa maji vijiji vya Shongo na Igale maelfu wafurahia. Katika ziara hiyo kaagiza wakala wa visima (DDCA) kuchimba kisima kirefu kijjiji cha Mjele kutekeleza ahadi ya mhe Rais Jakaya Kikwete kuwaokoa wananchi maelfu kufuata maji umbali wa kilomita 7. Pia ametoa ahadi ya kuanza utekelezaji wa mradi wa maji wa maji vijiji vya Iwindi,Mwashiwawala na Izumbwe ambao ulisimama baada mkandarasi kusimamishwa kwa kushindwa kazi.
Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akikwepa utelezi wakati akikagua chanzo cha maji ya chemchemu ya Ndoba kijiji cha Galijembe
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akipokea zawadi kijiji
cha Shongo
ambako wananchi wakimlaki kwa furaha
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla katika Akipanda mti
chanzo cha Ndoba- kijiji cha Galijembe
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akizindua rasmi mradi kijiji cha shongo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kuna jamaa nyuma amebana pua inaonekana kuliwa na harufu kali.
ReplyDeleteMh. Naibu Waziri yabidi uwe na mtu wa dressing, unapoenda site huendi umevaa Safari Suit, vaa jeans, kadeti na Tshirt, kofia na buti au raba.
ReplyDeleteKuhusu mavazi hayo ni maamuzi ya mtu binasfi, sio lazima aige wengine wanavaaje? Tusiingilie uhuru wa mtu. Mh. Makalla vaa unavyojisikia, hiyo ndio multicultural.
Deletewee anon, kuhusu jamaa aliyebana pua, umeniacha hoi!!!!
ReplyDeleteWill he declare zat gift?
ReplyDeletenchini UK kuna chombo maalumu cha kukagua zawadi wanazopewa viongozi wa nchi pamoja na wafanyakazi wa umma ili zisiweze kuwabadili katika kufanya wajibu wao waliopewa na maamumzi makubwa. Hii ni kwa zawadi zote wanazopewa wakiwa ndani ya nchi na nje ya nchi na kiongozi akishindwa kulipoti zawadi yoyote aliyopewa anapewa hukumu.
ReplyDeleteSwali, Mnaonaje hiki chombo kikaanzishwa Tanzania??
Viongozi wawe na uwezo wa kusoma mazingira, kila sehemu na nguo zake, sasa unaendaje site na suti na mokasini? SEPARATION OF PAMBA IZINGATIWE
ReplyDeleteKayamba mtu hapo
ReplyDelete