Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla amefanya ziara ya vijiji mbalimbali Mbeya Vijijini ambako amezindua mradi mkubwa maji vijiji vya Shongo na Igale maelfu wafurahia. Katika ziara hiyo kaagiza wakala wa visima (DDCA) kuchimba kisima kirefu kijjiji cha Mjele kutekeleza ahadi ya mhe Rais Jakaya Kikwete kuwaokoa wananchi maelfu kufuata maji umbali wa kilomita 7. Pia ametoa ahadi ya kuanza utekelezaji wa mradi wa maji wa maji vijiji vya Iwindi,Mwashiwawala na Izumbwe ambao ulisimama baada mkandarasi kusimamishwa kwa kushindwa kazi.
Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akikwepa utelezi  wakati akikagua chanzo cha maji ya chemchemu  ya Ndoba kijiji cha Galijembe
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akipokea zawadi kijiji cha Shongo
ambako wananchi  wakimlaki kwa furaha 
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla katika Akipanda mti chanzo cha Ndoba- kijiji cha Galijembe
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akizindua rasmi mradi kijiji cha shongo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kuna jamaa nyuma amebana pua inaonekana kuliwa na harufu kali.

    ReplyDelete
  2. Mh. Naibu Waziri yabidi uwe na mtu wa dressing, unapoenda site huendi umevaa Safari Suit, vaa jeans, kadeti na Tshirt, kofia na buti au raba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuhusu mavazi hayo ni maamuzi ya mtu binasfi, sio lazima aige wengine wanavaaje? Tusiingilie uhuru wa mtu. Mh. Makalla vaa unavyojisikia, hiyo ndio multicultural.

      Delete
  3. wee anon, kuhusu jamaa aliyebana pua, umeniacha hoi!!!!

    ReplyDelete
  4. Will he declare zat gift?

    ReplyDelete
  5. nchini UK kuna chombo maalumu cha kukagua zawadi wanazopewa viongozi wa nchi pamoja na wafanyakazi wa umma ili zisiweze kuwabadili katika kufanya wajibu wao waliopewa na maamumzi makubwa. Hii ni kwa zawadi zote wanazopewa wakiwa ndani ya nchi na nje ya nchi na kiongozi akishindwa kulipoti zawadi yoyote aliyopewa anapewa hukumu.

    Swali, Mnaonaje hiki chombo kikaanzishwa Tanzania??

    ReplyDelete
  6. Viongozi wawe na uwezo wa kusoma mazingira, kila sehemu na nguo zake, sasa unaendaje site na suti na mokasini? SEPARATION OF PAMBA IZINGATIWE

    ReplyDelete
  7. Kayamba mtu hapo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...