Mmoja wa waasisi na viongozi wakongwe wa CCM Hajat Kijakazi Salum Kyerula amefairiki dunia jijini Dar es salaam jana. Taratibu za mazishi zinafanyika mikocheni eneo la Victoria karibu na Oil com pamoja na hospitali ya Kairuki, jijini Dar es salaam. Swala ya maiti itafanyika hapo hapo Mikocheni sambamba na swala ya Ijumaa na baadaye maziko yatafanyika Mtoni Kijichi, kwenye makaburi ya njia panda ya Neruka.
WASIFU WA MAREHEMU
HAJAT KIJAKAZI SALUM KYELULA NA RATIBA YA MAZISHI
Hajat
KIJAKAZI SALUM KYELULA alizaliwa tarehe 1/1/1941, katika uhai wake
amefanya kazi Radio Tanzania(TBC), Shirika
la Habari la Tanzania (SHIHATA). PIA Marehemu kijakazi amewahi kuwa mwenyekiti wa Umoja
wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya
Ilala. katibu mkuu wa CCM mkoa wa Morogoro na Kilimanjaro kwa vipindi tofauti.
Marehemu
amekuwa Mbunge wa Taifa kwa takribani miaka 15, Naibu Waziri
Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Pamoja na nafasi hizo Bi.
Kijakazi ni mwanzilishi wa umoja wa kina
mama wa Regent (Regent Women Neighbourhood -
REWONE), umoja wa kina mama wa
kiislamu MIKOCHENI(SAFINA), na pia alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa msikiti
wa Regent Estate.
Marehemu ameacha watoto 7 ,wajukuu 14 na
vitukuu viwili.
Innalilah wainailalai Rajiun
RATIBA YA
MAZISHI LEO MTONI KIJICHI, DAR ES SALAAM
TUKIO
|
MUDA
|
MUHUSIKA
|
KISOMO(SURAT RAHMAN & SURAT YASSIN)
|
SAA
5:00 ASUBUHI
|
ABDALLAH
KIONGA
|
WASIFU
WA MAREHEMU
|
SAA
5:50 ASUBUHI
|
RAMADHANI
KITWANA
|
SADAKA
|
SAA
6:OO MCHANA
|
|
KUELEKEA
MSIKITINI KWA SALAT JUMAA NA SALAT JANAIZA
|
SAA
6:45 MCHANA
|
ABDALLAH
KIONGA
|
MSAFARA
KUELEKEA MTONI KIJICHI
|
SAA
7:15 MCHANA
|
MJOMBA
MSAKUZI
|
MSAFARA
KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KIJICHI KWA SALAT JANAIZA NA KISHA KUELEKEA
MALALONI
|
SAA
8:15 MCHANA
|
MJOMBA
HAJJI
|
Innalillah wajnarajuun...
ReplyDeleteMwenyezi mungu amjaalie amfanyie wepesi katika safari yake hii na amsamehe makosa yake amin
na ampe kauli dhabit hakika sisi binaadam kwa allah ndio marejeo yetu
na wafiwa poleni sana allah atawapeni nguvu katika kipindi hichi kizito sana kwenu...amin
Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiuna. Mwenyeez Mungu akulaze pema peponi Bi Kijakazi Salum Kyerula - Ameen. Akughufirie kwa yote, akunusuru na adhabuze zote za dunia, za kaburi na za kesho akhera. Akupumzishe katika kivuli chake na kesho uwe ni miongoni mwa waja wake wema watakaoingia katika yaje Jannatu N'naeem. In Sha Allah - AMEEN.
ReplyDeletePoleni ndugu, jamaa na marafiki wote mliofikwa na kuguswa na msiba huu. Poleni sana.
Innaa lillaahi wainnaa ilayhi raajiun.Allahumaghfirlahaa waaskinha fil jannati.haya mambo ya uzushi uzushi ya visomo,sijui ratiba tuachane nayo jamani.tufate sunnah ya mjumbe wa Allah
ReplyDelete