Wapo Watanzania ambao ndoto zao ni kumiliki shule. Ninapoongelea shule simaanishi lazima yawe yale mashule makubwa. Hata shule za awali ambazo zinaanzishwa na wajasiriamali wadogo mitaani nazo ni shule kwa maana hii katika makala haya.
Nyaraka kuu inayoongoza taratibu za usajili wa shule binafsi huitwa fomu namba RS8. Huu ndio mwongozo mkuu wa usajili.
Kuna mambo ya msingi na ya kisheria ambayo mtu hutakiwa kujiandaa nayo iwapo anataka kuanzisha shule binafsi.
Mambo haya huwa yanakamilishwa kwa wepesi na bila usumbufu ikiwa yanapitia kwa wanasheria lakini pia mtu anaweza kufanya mwenyewe isipokuwa hata akifanya mwenyewe kuna document za lazima ambazo lazima zisainiwe na kuthibitishwa na mwanasheria.
Hizi makala za sheria ni makala muhimu sana sana...asante michuzi na team yako.
ReplyDeletemaoni...napendekeza kuwepo na urahisi wa kuzisearch zile zilizopita yaani kama direct link fulani ya kuzisoma zote..mfano ile sehemu ya kumbumbuku badala ya kuweka kimwezi mwezi pia unaweza ongeza kimakala au aina ya habari..bila shaka kiswahili changu kimeeleweka.
Niwashukuru tena
Mdao wa blog