Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye zoezi la kuipigia kura Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mwito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika tawi la Msinjahili wilayani humo.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema zoezi la uandikishaji litafanyika kwa muda wa wiki moja na katika mkoa huo litaanza tarehe 16 hadi 22 mwezi huu hivyo basi ni muhimu wananchi wakajitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya msingi ya kujiandikisha.
“Mkoa wetu ni mmoja kati ya mikoa minne ya mwanzo itakayoanza zoezi hili, mikoa mingine ni Mtwara, Ruvuma na Njombe. Ni muhimu wananchi mkajitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani uandikishaji utafanyika kwa njia ya mashine na baada ya wiki moja mashine hizi zitahamia katika mkoa mwingine”, alisema Mama Kikwete.
Ingekuwa vyema kama ungehamasisha wananchi wa nchi nzima wajiandikishe au angalau katika mikoa yote minne ambayo zoezi hili linaanzia na si Lindi peke yake. Kumbuka wewe ni first lady wa JMT na si lindi.
ReplyDelete