Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Januari, 2015 leo jijini Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2015 umepungua hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.8 ya mwezi Desemba, 2014 kutokana na kuendelea kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa na huduma mbalimbali nchini.
Akitoa taarifa ya mfumuko huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kupungua kwa mfumuko wa Bei katika maeneo mbalimbali nchini kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na zile zisizo.
Amesema kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya kimeonyesha kupungua katika maeneo mbalimbali nchini kikihusisha bei ya mahindi, Unga wa mahindi , ndizi, ndizi za kupika na mihogo.
Mambo ya kushangaza. Sijui huko mikoani bei za bidhaa zikoje lakini kwa hapa Dsm, bei za vyakula hazijashuka bali zimepanda. Kwa mfano bei ya mchele, maharagwe, sukari hazijashuka bali zimepanda. Kwa hivyo taarifa za huyo mataalamu kuhusu mfumuko wa bei zinatia shaka.
ReplyDelete