Na Amon Mtega - Songea
MTOTO Sophia Abdul (14) anayesoma shule ya msingi Lilahi darasa la tano
iliyopo kata ya Mhukulu wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma
amekumbwa na ugonjwa usiofahamika ambao umejitokeza kwenye jicho lake
la kulia lililo vimba na kutokezea nje hali inayomletea maumivu makali
na kushindwa kwenda shule huku akiomba msaada kwa wasamalia wema.
Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za elimu za wilaya hiyo mama wa mtoto huyo Joyce Nyoni alisema kuwa mwanae alianza kupatwa na ugonjwa huo toka Aprili mwaka jana lilianza kuwasha kisha kujitokeza uvumbe ambao umepelekea jicho hilo kushindwa kuona huku likiwa limetoka kwa nje.
Alisema baada ya kuona hali ya mwanae inazidi kuwa mbaya alimpeleka katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kukutana na madaktari ambao walimwambia kuwa ugonjwa huo hawatauweza badala yake walimtaka atafute fedha ampeleke katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili.
Joyce aliongeza kuwa baada ya kupata maelekezo ya madaktari aliamua kupita kuomba msaada kwa wasamalia wema ili kunusuru maisha ya mwanane kwa kuwa yeye mwenyewe hana uwezo wa kifedha na kwamba baba wa mtoto huyo Abdul Rashid alimtelekeza toka akiwa na umri wa mwaka mmoja.
Alisema kufuatia hali hiyo mwanae hajahudhulia masomo toka walipofungua shule jambo ambalo linaweza kumrudisha nyuma katika maendeleo yake na haki ya kupata elimu,hata hivyo aliambiwa na madaktari hao kuwa pindi atakapopata fedha za matibabu watamwandikia kibari cha kumruhusu kwenda kupata matibabu Muhimbili.
Aidha mama wa mtoto huyo anawaomba wasamalia wema kutoa mchango wao wa hali na mali ili afanikiwe kumpeleka mwanae kwenye matibabu,kiwango cha fedha kinachohitajika hadi sasa hajafahamu baada ya kupewa kibali atafahamishwa kwa watakao guswa na tatizo la mtoto Sophia watoe michango yao kwa simu namba 0683115075 ya mama yake.
Maa shaa allah, Mungu ampe tahfifu mtoto huyu na amfanyie wepesi katika kupata matibabu in shaa allah. Nafkiri kikubwa ni kupata nauli ya kumfikisha Dar.
ReplyDeletenajaribu kupiga simu ya huyo mama haipatikani. kwa atakayempata, amweleze aende hospitali ya rufaa Mbeya kati ya Jumatatu 23 hadi jumatano 25 kuna program ya macho kwa watoto toka Muhimbili, wagonjwa wanaopatikana hapo wanapata uchunguzi na matibabu ikibidikusafirishwa kwenda Muhimbili. kwa UFADHILI WA program ya SEEING IS BELIVING. ASISAHAU KARATASI YAKE YA RUFAA.
ReplyDelete