FAITH CATHERINE GONDWE |
FAMILIA YA BW. GEOFFREY GONDWE YA BAHARI BEACH, DAR ES SALAAM, INAPENDA KUWASHUKURU WATU
WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AMA INGINE KATIKA KUHITIMISHA SAFARI YA MWISHO
YA MTOTO WAO FAITH CATHERINE GONDWE ALIYEFARIKI DUNIA GHAFLA SIKU YA JUMANNE FEBRUARY
17, 2015 JIJINI DAR ES SALAAM, NA KUPUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE SIKU
YA JUMAMOSI FEBRUARY 21, 2015 KATIKA MAKABURI YA KINONDONI.
FAMILIA YA BW. GEOFFREY GONDWE INATAMBUA KWAMBA SI RAHISI
SANA KUMSHUKURU MTU MMOJA MMOJA KWA MSAADA WA HALI NA MALI ALIOTOA KWAO KATIKA
WAKATI HUU MGUMU, ILA NI MUHIMU KUTAMBUA MCHANGO MKUBWA ULIOTOLEWA NA KANISA LA
ST. GASPER LA MBEZI BEACH, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA JIRANI WA FAMILIA, BILA
KUASHAU USHIRIKIANO WA KARIBU SANA ULIOTOLEWA NA MWAJIRI WA MAREHEMU FAITH
(TANESSCO) PAMOJA NA WANACHAMA JAMBO BROTHERS WA KUNDUCHI JIJINI DAR ES SALAAM.
BABA WA MAREHEMU, BW. GEOFFFREY GONDWE, AMBAYE
YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU, NA MKEWE, PAMOJA NA FAMILIA NZIMA YA GONDWE KWA
UJUMLA WANATOA AHSANTE NYINGI SANA KWA KILA ALIYESHIRIKI NAO KATIKA MSIBA WA
BINTI YAO KIPENZI, FAITH.
KWA PAMOJA FAMILIA YA GONDWE WANASHUKURU KILA MTU NA KUSEMA
KWAMBA MUUMBA WA YOTE MWENYEZI MUNGU AWAJAALIE NA KUWAONGEZEA WALIPOPUNGUKIWA.
FAMILIA YA GONDWE WANASEMA KUONDOKA KWA FAITH NI KUDURA ZAKE
BWANA KWANI NDIYE ALIYELETA NA NDIYE ALIYETWAA. HIVYO KUDURA ZAKE NA ZIHIMIDIWE.
- AMINA
Jamani kwanza napenda kusema poleni kwa msiba huo mkubwa,Halafu naomba mniambie kama huyu dada pia alikuwa anaitwa Eliwaza Samweli kwenye akaunti yake ya facebook.maana wanafanana sana sura zao Huyo Faith na huyu Eliwaza ilinijua kama ni huyu rafiki yangu wa kwenye facebook ndiye aliye nitoka au ni tofauti.
ReplyDeleteI am praying for the family. May God give strength
ReplyDelete