FAITH CATHERINE GONDWE
FAMILIA YA BW. GEOFFREY GONDWE YA BAHARI BEACH, DAR ES SALAAM, INAPENDA KUWASHUKURU WATU WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AMA INGINE KATIKA KUHITIMISHA SAFARI YA MWISHO YA MTOTO WAO FAITH CATHERINE GONDWE ALIYEFARIKI DUNIA GHAFLA SIKU YA JUMANNE FEBRUARY 17, 2015 JIJINI DAR ES SALAAM, NA KUPUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE SIKU YA JUMAMOSI FEBRUARY 21, 2015 KATIKA MAKABURI YA KINONDONI.
FAMILIA YA BW. GEOFFREY GONDWE INATAMBUA KWAMBA SI RAHISI SANA KUMSHUKURU MTU MMOJA MMOJA KWA MSAADA WA HALI NA MALI ALIOTOA KWAO KATIKA WAKATI HUU MGUMU, ILA NI MUHIMU KUTAMBUA MCHANGO MKUBWA ULIOTOLEWA NA KANISA LA ST. GASPER LA MBEZI BEACH, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA JIRANI WA FAMILIA, BILA KUASHAU USHIRIKIANO WA KARIBU SANA ULIOTOLEWA NA MWAJIRI WA MAREHEMU FAITH (TANESSCO) PAMOJA NA WANACHAMA JAMBO BROTHERS WA KUNDUCHI JIJINI DAR ES SALAAM.
BABA WA MAREHEMU, BW. GEOFFFREY GONDWE, AMBAYE YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU, NA MKEWE,  PAMOJA NA FAMILIA NZIMA YA GONDWE KWA UJUMLA WANATOA AHSANTE NYINGI SANA KWA KILA ALIYESHIRIKI NAO KATIKA MSIBA WA BINTI YAO KIPENZI, FAITH.
KWA PAMOJA FAMILIA YA GONDWE WANASHUKURU KILA MTU NA KUSEMA KWAMBA MUUMBA WA YOTE MWENYEZI MUNGU AWAJAALIE NA KUWAONGEZEA WALIPOPUNGUKIWA.
FAMILIA YA GONDWE WANASEMA KUONDOKA KWA FAITH NI KUDURA ZAKE BWANA KWANI NDIYE ALIYELETA NA NDIYE ALIYETWAA. HIVYO KUDURA ZAKE NA ZIHIMIDIWE.
 - AMINA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamani kwanza napenda kusema poleni kwa msiba huo mkubwa,Halafu naomba mniambie kama huyu dada pia alikuwa anaitwa Eliwaza Samweli kwenye akaunti yake ya facebook.maana wanafanana sana sura zao Huyo Faith na huyu Eliwaza ilinijua kama ni huyu rafiki yangu wa kwenye facebook ndiye aliye nitoka au ni tofauti.

    ReplyDelete
  2. I am praying for the family. May God give strength

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...