Ulikuwa ni usiku wa manane majira ya saa nane na nusu, ambapo Mzee
Jengo alikuwa amepumzika kitandani akiwa na mtoto wake wa kiume ambaye alikuwa
anaitwa Rony.
Alikuwa ni kijana mdogo mwenye umri
kati ya miaka nane au tisa, Usiku huo hali ya Mzee Jengo ilikuwa si
nzuri kwani alianza kujisikia vibaya ghafla kiasi kwamba hata alipojaribu
kunyanyuka alishindwa. Kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyasikia aliamua
kumuamsha mtoto wake, taratibu alinyoosha mkono na kuanza kumvuta Ronyhuku
akizungumza kwa sauti ya unyonge sana.
“Rony, Rony
…..aaaaa…amka ukamwambie ….dada mimi naumwa, Rony mwanangu nenda kamwite dada
yako najisikia vibaya sana” Alikuwa akizungumza kwa shida sana, lakini Rony
alimsikia, na kwa haraka aliamka huku akiwa anafikicha macho yake kutokana na
kushtuka kutoka usingizini, alimtizama baba yake, na moja kwa moja alishuka
kutoka kitandani huku akiwa anamuuliza Baba yake, “Baba unaumwa nini, nani atakupeleka hospitali Baba,”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...