Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe (pichani) usiku huu ametangaza rasmi Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia CHADEMA.
Mhe. Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.
Juu Mheshimiwa Zitto Kabwe na wabunge wengine wakitoka Bungeni mjini Dodoma leo. Chini akiwa na Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe (kuhoto) na Mbunge mwingine
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba Mungu akipenda atakuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo hii hapa...
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba Mungu akipenda atakuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo hii hapa...
Michango yako Mh. Zitto kwa taifu letu ni kubwa sana!
ReplyDeleteNaomba, nipendekeze kwa Mh. Rais kama ataweza kumteua ZK kama Mbunge wa Kuteuliwa [Nominated MP] kulingana na Ibara 46(1) ya Katiba letu tukufu ya mwaka 1977.
Tujikumbushe kwamba, hivi sasa tuna wabunge wa kuteuliwa nane wakiwemo:
*Zakia Meghji [2010]
*Prof. Makame Mbarawa [2010]
*Shamsi Vuai Nahodha [2010]
*Saada Salum [2012]
*Janet Mbene [2012]
*Prof. Sospeter Muhongo [2012]
*James Mbatia [2012]
*Dr Asha Migiro [2013]
Kwa hiyo, kabla ya Bunge la 10 kuvunjika; Mh. Rais anaweza kuwateua Mwanamke na Mwanaume mmoja!
Wadau mnasemaje? Nawasilisha hoja..
Naomba nijisahihishe:
ReplyDeleteNilikosea hapo juu. Ibara sahihi ni 66(1)(e) na sio 46(1).
Samahani kwa usumbufu.
http://www.judiciary.go.tz/downloads/constitution.pdf
Nakuhunga Mkono Ndugu ALI... Kwenye katiba mpya kuna mabadiliko ya kifungu hiki kwani.Nchi kama Uingereza kifungu hiki kimewekwa kuwa kama unatoka utatolewa kwenye chama unakuwa huru. Na unaweza kuwa bado mbunge kwani umechaguliwa na wananchi kuwawakilisha na kwenye demokrasia nafikiri kitu kama hiki kinatakiwa kupewa kipaumbele sana.
ReplyDeleteHili ni jembe...pumzika jembe but i know you will come back strongly like an injured tiger!!bongo watu kama nyie mko wachache sana na mnapigwa vita...hongera jembe umeondoka kishujaa.Big up!!
ReplyDeleteMdau wa Oxford,UK,
MIMI NAMSHAURI MH. ZZK AGOMBEE TENA UBUNGE KATIKA LILE JIMBO LAKE KUPITIA CHA CHOCHOTE KINGINE LAKINI ISIWE C.C.M. AU CHADEMA NA ATAPITA TU KWASABABU KAZI YA KIJANA HUYU TUMEIONA.
ReplyDeleteWanapashwa kuacha kuchagua watumishi wa serikali na wizara kutoka kwa wabunge.
ReplyDeleteHuu ndiyo unaitwa ukomavu wa kisiasa.
ReplyDeleteMbunge aliyefukuzwa ubunge kukubali kungatuka ubunge na pia chama kilichomvua uanachama kuhakikisha kuwa katiba,kanuni na taratibu za chama zinafuatwa.
Hongereni wadau wote yaani mbunge ambaye ni mwanachama yaliyefukuzwa na chama cha CHADEMA kwa kuzingatia taratibu, kanuni na katiba mlizojiwekea.
Mdau
Diaspora
hiyo poa kabisa. JK Changamka bwana!
ReplyDeleteYataka moyo na unyenyekevu, kufukuzwa na kuja mbele ya wabunge wenzako kuaga. Huo ni moyo wa kishujaa sana. Hongera, na mpende Mungu atakujalia tena unayohitaji hapo baadaye. Bye MH ZZK
ReplyDeleteNi kweli kabisa
ReplyDeleteKuwa rais wa Tz ni rahisi kuliko kuwa mwenyekiti wa Chadema. vita yake kubwa kuliko kupiga kampeni ya uraisi.
ReplyDeleteNapenda kukupinga kwa nguvu zote mchangiaji wa kwanza ETI ndg Zitto arudishwe bungeni kama mbunge wa kuteuliwa..
ReplyDeleteZZK ni jembe la nguvu halihitaji hisani ya rais ili aweze kurudi bungeni, wananchi wa jimboni kwake wanamtaka na watanzania wengi wanampenda pia kwa hio he will be back bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi tena hahitaji hisani ya rais kumchagua hao wote uliowaweka hapo wamo bungeni kwa vile hawachaguliki na kuwalinganisha na jembe langu ZZK please give him a break.. muache apumzike ajipange vizuri Chadema sio baba yake au mama yake..nawakilisha.
Asante Bw. Ally Ahmed kwa maoni yako. Naomba nikuulize: Kweli ZK ataweza kurudi tena ndani ya Bunge la 10? Hawezi kwasababu hatutakuwa na uchaguzi mdogo [by-election] kulingana na Elections Act of 1985 [Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985]. Ndio maana, pia, hatuna uchaguzi mdogo jimboni Mbinga Magharibi kwa Marehemu Capt. Komba.
ReplyDeleteUkitaka ZK arudi ndani ya Bunge hili kabla haijavunjwa mwezi [nadhani] July; ni njia mmoja tu: Kwa kuteuliwa! Rais anaweza kumteua; na vile vile ZK anweza kukataa uteuzi kama anataka kupumzika kidogo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka. Ila, akikubali, itabidi ajiunge na chama cha siasa kingine ili aweze kuteuliwa kwa mujibu wa katiba yetu kinachotuongoza hivi sasa.