Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoishi kwenye Hostel za Mabibo,wakiangalia moja ya majengo ya Hostel hizo likiwa limeshika moto asubuhi hii.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na msaada wa haraka unahitajia ili kuokoa mali zilizopo kwenye Jengo hilo.
Hakuna anaeamini anachokiona,kwani imekuwa ni tukio la ghafla sana.
Baadhi ya Wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye Jengo hilo wakiwa nje,huku wakiwa hawajui la kufanya wakati moto huo ukiendelea kuwaka.
Moshi unazidi kufuka na moto unaongezeka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Je fire extinguishers zipo?,water sprinkles zipo kila floor? fire drills zimekuwa zikifanyika kujitayarisha na moto? je kuna meeting point zinazoeleweka...Hii ni kabla hatujaangalia jiji linasaidia je katika swala zima la zima moto..

    ReplyDelete
  2. Je majengo haya yamelipiwa bima ya moto?

    ReplyDelete
  3. madesa yangu yameungulia hosteli ndo maana mtihani umemshinda.

    ReplyDelete
  4. Poleni ndugu zetu! ! mungu atawapa nguvu na sisi Watanzania Tupo nyuma yenu na tunawategemea kama rasilimali ijayo. Elimu juu ya maafa kama moto inahitajika sana hasa mashuleni na vyuoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...