Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank Plc Bw. Edmund Mkwawa akiongea na Waandishi wa Habari Makao makuu ya Benki ya DCB
Benki ya DCB imethibitisha kushiriki katika Mashindano ya Tanzania Bankers and Public Funds Cup 2015, hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bwana Edmund Mkwawa akiongea na waandishi wa Habari , alisema Timu yao tayari imesha anza kufanya mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo tangu mwezi wa pili mwaka huu 2015 na kuwa timu ipo katika hari nzuri sana si kwa kushiriki tuu lakini pia kutoa upinzani mkubwa watakazokutana nazo na hata kunyakua kikombe.
Pia Bwana. Mkwawa amesema kuwa DCB pamoja na kushiriki kwao lakini wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuweza kufanikisha kwa ufasaha zaidi na kuongeza kuwa lengo kubwa la DCB Commercial Bank kupitia udhamini na ushiriki wa mashindano hayo ni kupanua wigo mkubwa wa kimahusiano na kibiashara kwa ukaribu zaidi baina ya Benki,Mifuko ya kijamii na Jamii kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...