Katika
adhima ya kufikisha mawasiliano vijijini, Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL) imezindua mnara wa mawasiliano ya simu katika kata ya Pagwi,
wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga.
Akihutubia
mamia ya wananchi waliohudhuria tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi
Selemani Liwowa alisema kwa kupata mawasiliano itasaidia wananchi
kuwasiliana pamoja na kutafuta fursa mbalimbali kwa ajili maendeleo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya alisisitiza wananchi kutumia mawasiliano ya simu
kwa ajili ya shughuli za maendeleo na usalama wa mali zenu pamoja na
nchi kwa ujumla.
“Nawaombeni
pia tumieni fursa hii ya uwepo wa mawasiliano kwa ajili ya kukuza
uchumi wa Kata hii, kutafuta masoko nje na ndani ya mkoa wa Tanga”
alisema Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa.
Naye
Meneja wa TTCL mkoa wa Tanga alisema kuwa mnara huo unatoa huduma ya
mawasiliano katika vijiji vya Lumotio, Pagwi, Makelele, Masilei, Kwekivu
na maeneo yote yanayozunguka vijiji hivyo.
Lusama
alifafanua kuwa kupitia mfuko unaosimamia utoaji wa huduma ya
Mawasiliano kwa wote nchini (UCSAF), TTCL ilipewa jukumu la kufikisha
huduma za mawasiliano katika kata 20 kwa awamu ya kwanza ya utekelezaji
wa mradi wa mawasiliano vijijini. Katika Kata hizo za mwanzo Pagwi ni
moja ya Kata zilizonufaika na mradi huo.
Meneja
wa Mkoa wa Tanga wa TTCL, Peter Lusama akitoa hotuba siku ya Uzinduzi
wa Mnara wa Mawasiliano katika kata ya Pagwi, Wilaya ya Kilindi, Tanga.
Mgeni
Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa akizungumza na
wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano wa Pagwi,
Wilaya ya Kilindi, Mkoani Tanga. Mnara huu umesaidia wananchi wa maeneo
hayo kupata mawasiliano ya simu.
Mgeni
Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa akikata utepe,
kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasiliano wa Pagwi, Wilaya ya
Kilindi, Tanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...