Na Bakari Issa,Dar es Salaam

Kampuni ya Ask Indus (T) Limited yenye lengo la kuunganisha kati ya Tanzania na India katika nyanja ya Afya,elimu pamoja na masuala ya biashara hususan katika sekta binafsi imezinduliwa rasmi leo,nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam,Balozi wa India nchini,Mhe. Debnath Shaw amesema Watanzania watafaidika na Kampuni hiyo kwa kuwa itatoa msaada zaidi katika matibabu bora,Elimu bora kwa wanafunzi pamoja na huduma bora zaidi za kibiashara kwa Wafanyabiashara.

Aidha,Shaw ameishukuru nchi ya Tanzania kwa ushirikiano mpaka kuanzishwa kwa Kampuni hiyo ambayo itawasaidia Watanzania,pamoja na kuunganisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Naye,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ask Indus,Bw.Abhilash Puljal amemshukuru Balozi wa India nchini kwa kukubali wito wa kuja ili kufanya uzinduzi wa Kampuni hiyo itakayowasaidia Watanzania kupata huduma bora ya Afya,Elimu pamoja na biashara nchini India.

Kampuni ya Ask Indus (T) Limited ina matawi mengine katika nchi za India,Kenya,Mauritius pamoja na Nigeria.
Balozi wa India nchini,Mhe. Debnath Shaw (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kampuni ya Ask Indus itakayojihusisha na masuala ya utoaji huduma za Afya,Elimu pamoja na biashara,uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ask Indus,Bw.Abhilash Puljal.
Balozi wa India nchini,Mh. Debnath Shaw (aliyesimama) akizungumza jambo kwa wadau kuhusu Kampuni ya Ask Indus ambayo itajihusisha na utoaji huduma za Afya,Elimu pamoja na biashara,iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Ask Indus,Bw. Abhilash Puljal (katikati) na kulia ni Msimamizi wa Tawi la Tanzania,Bw. Prakash.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ask Indus,Bw.Abhilash Puljal (kulia) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kampuni yake hiyo yenye lengo la kuunganisha kati ya Tanzania na India katika nyanja ya Afya,elimu pamoja na masuala ya biashara hususan katika sekta binafsi uliofanyika jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wakisikiliza kwa umakini juu ya tukio la uzinduzi wa Kampuni ya Ask Indus (T) Limited.Picha na Emmanuel Massaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwanza, India ituunganishe na ndugu zetu walioko huko Ingia. yaani kabila la Sidi. Wengine walichukuliwa na kuuzwa utumwani; wengine walikuwa ni wafanyabiashara tangu karne ya nyingi.

    ReplyDelete
  2. TWILA KAMBANGWAMarch 24, 2015

    yes mdau wale ni ndugu zetu kabisa wana sidi wanatokomezwa na hawa wadosi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...