Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto) akimsikiliza Naibu Meya, Songoro Mnyonge wakati akimpa maelezo kuhusu mazingira ya Mto Kiboko uliopo katika Kata ya Tandale wakati wa ziara yake katika Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana.
Mkazi wa Mtaa wa Bahi, Jomo Macha akimueleza Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda athari za mafuriko katika Mtaa huo, Kata ya Makumbusho wakati wa ziara ya Meya huyo jana. Wengine ni Watendaji wa Manispaa hiyo na wakazi wa eneo hilo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akitoa maelekezo kwa watendaji wa Manispaa hiyo kuhusu kutafuta ufumbuzi wa chemba ya majitaka iliyofurika katika Mtaa wa Balozi Msolomi wakati wa ziara yake. Kulia kwake ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na watendaji wa Manispaa hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (mbele) akikagua mto Ng'ombe uliopo eneo la Mwananyamala Kisiwani, wakati wa ziara hiyo Nyuma yake ni Naibu Meya,Songoro Mnyonge.
Eh Mheshimiwa Meya hivi unakwenda kutembelea maeneo ya mafuriko na buti hiyo kali na suti?
ReplyDeletesielewi viongozi kwanini hawavai kuendana na matukio...unaendaje kwenye mafuriko na suti na moka?
ReplyDeleteNi lini nchi yetu viongozi wataacha kuwa wa kutembelea maafa(aftermath) na kuwa viongozi wa kuzuia maafa kwa kuweka na kutekeleza mipango endelevu?
ReplyDeleteHiyo sehemu ina ule uchafu uliokithiri ambao ni vigumu kuelewa kwanini uko hapo.
ReplyDelete