Benki ya NMB imemkaribisha Mkurugenzi Mtendaji mpya – Ineke Bussemaker anayechukua nafasi ya Mark Wiessing aliyemaliza muda wake.
Mark Wiessing amepangiwa kituo kingine cha Kazi ndani ya Benki Mama ya NMB – ‘Rabobank’ na sasa ataenda kuwa Meneja Mkuu nchini Brazil.
Bwana Wiessing ataanza rasmi wadhifa mpya mwezi wa tano mwaka huu.
Ineke Bussemaker anakuja NMB akitokea ndani ya shirika mama la NMB – ‘Rabobank’ la nchini Uholanzi ambako alikuwa Mtendaji Mkuu katika Kitengo cha Malipo.
Ineke ana uzoefu wa juu wa masuala ya kibenki na biashara ya kimtandao, utaalamu ambao unaelezwa kuwa utaisaidia benki ya NMB kukua zaidi.
Kabla ya RaboBank, Ineke alishika nyadhifa mbalimbali za juu katika banki za Citibank, ABN Amro Bank ya uholanzi, Uingereza na Denmark.
Mark Wiessing anaiacha NMB ikiwa imekuwa kwa kasi kwa miaka minne ya uongozi wake, ameiacha NMB ikiwa na matawi zaidi ya170 na ATM zaidi ya 600 nchi nzima, huku ikiwa na hazina ya wateja zaidi ya milioni mbili, ambapo faida imekuwa kwa kasi kutoka Shilingi Bilioni 54 (Baada ya Kodi) mwaka 2010 mpaka faida ya Shilingi Bilioni 155 baada ya kodi mwaka 2014.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker akisalimiana na naibu gavana wa benki kuu ya Tanzania (BOT) – Juma Reli katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker akitoa hotuba fupi kwa wageni waalikwa, uongozi wa juu wa benki na bodi ya wakurugenzi wa NMB katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker katika mazungumzo na meya wa Ilala – Jery Silaa na Mwenyekiti wa Bodi ya NMB – Prof Joseph Semboja katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
Mwenyekiti wa Bodi ya NMB – Prof Joseph Semboja akiongea wakati wa katika hafla iliyofanyika na NMB kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Bw. Mark Wiessing (kushoto) akiongea na waalikwa katika hafla ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
I had an unforgettable experience with the NMB last November as in "The Year 2014 and my re-introduction to life by the National Microfinance Bank" I truly wish the Bank well. It has much to do in changing attitudes and catching up with the times. I know it can. It has has no choice if it is to earn the confidence and trust of its clients.
ReplyDelete