Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili, Machi 29, 2015 amewasili jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Umoja wa Mataifa.

Miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete amefunguia rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa, na Jumatatu Machi 30, 2015 amealikwa kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (ECOSOC - UN).
Rais Kikwete akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa Dkt Mahadhi Juma Maalim alipowasili jijini New York, Marekani. 
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa WAZIRI wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka anayefuatiwa na Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee ...
Jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...