Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya watu walioathirika na Ukimwi vinatokana na Ugomjwa wa Kifua Kukuu na inakadiriwa  kuwa tangu kuanza  kwa ugonjwa wa ukimwi, kati ya asilimia tano (5) hadi 10 ya watu wenye VVU wana ugonjwa wa kifua kikuu  na takribani ya asilimia 40 wanaouguwa  kifua kikuu  wana maambukizo ya VVU.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Donan Mmbando wakati akitangaza maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijni Dar es Salaam ambayo hufanyika Machi 24 kila  mwaka .

Dk.Mmbando amesema, Tanzania ni nchi ya Sita katika bara la Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu na takwimu za Wizara ya Afya ziligundua kuwepo kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu zaidi ya 65,000 kwa mwaka 2013,utafiti wa mwaka 2012  wa kutathimini kiwango cha ugonjwa huo,ulionyesha kuwa idadi kubwa ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huo.

Aidha amesema Kifua Kikuu ni ugonwa unaoambukiza na unasababishwa na vimelea aina ya bacteria na mtu anayeugua ugonjwa huo ni rahisi kuambikiza kwa watu wengine  kwa kukohoa au kupiga chafya.

Dk.Mmbando aliendelea zaidi kwa kumesema kwa sasa takribani zaidi ya watu milioni 1.5 duniani  wanafariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka na asilimia kubwa ya vifo hivyo vinatokea katika  nchi za Kusini  mwa Jangwa la sahara na Tanzania ni kati ya nchi 22 yeye idadi kubwa ya wagonjwa wa kifua Kikuu Duniani.

nchi hizo zinachangia asilimia 80 ya wagonjwa wa kifua kikuu ulimwenguni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt.Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Wizarani hapo leo Machi 23,2015.Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Margaret Mhando.
Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma,Dkt. Beatrice Mutayobya akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,leo Machi 23,2015 jijini Dar es salaam.Picha na Emmanuel Massaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wanaokohoa kwa muda zaidi ya wiki mbili pata ushauri wa madaktari utibiwe, dawa zipo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...