Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya watu walioathirika na Ukimwi vinatokana na Ugomjwa wa Kifua Kukuu na inakadiriwa kuwa tangu kuanza kwa ugonjwa wa ukimwi, kati ya asilimia tano (5) hadi 10 ya watu wenye VVU wana ugonjwa wa kifua kikuu na takribani ya asilimia 40 wanaouguwa kifua kikuu wana maambukizo ya VVU.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Donan Mmbando wakati akitangaza maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijni Dar es Salaam ambayo hufanyika Machi 24 kila mwaka .
Dk.Mmbando amesema, Tanzania ni nchi ya Sita katika bara la Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu na takwimu za Wizara ya Afya ziligundua kuwepo kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu zaidi ya 65,000 kwa mwaka 2013,utafiti wa mwaka 2012 wa kutathimini kiwango cha ugonjwa huo,ulionyesha kuwa idadi kubwa ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huo.
Aidha amesema Kifua Kikuu ni ugonwa unaoambukiza na unasababishwa na vimelea aina ya bacteria na mtu anayeugua ugonjwa huo ni rahisi kuambikiza kwa watu wengine kwa kukohoa au kupiga chafya.
Dk.Mmbando aliendelea zaidi kwa kumesema kwa sasa takribani zaidi ya watu milioni 1.5 duniani wanafariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka na asilimia kubwa ya vifo hivyo vinatokea katika nchi za Kusini mwa Jangwa la sahara na Tanzania ni kati ya nchi 22 yeye idadi kubwa ya wagonjwa wa kifua Kikuu Duniani.
nchi hizo zinachangia asilimia 80 ya wagonjwa wa kifua kikuu ulimwenguni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt.Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Wizarani hapo leo Machi 23,2015.Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Margaret Mhando.
Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma,Dkt. Beatrice Mutayobya akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,leo Machi 23,2015 jijini Dar es salaam.Picha na Emmanuel Massaka.
Wanaokohoa kwa muda zaidi ya wiki mbili pata ushauri wa madaktari utibiwe, dawa zipo!
ReplyDelete