BENDI ya muziki wa kizazi kipya ya Yamoto Band na Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Omary Nyebo 'Ommy Dimpoz', kesho wanatarajiwa kuondoka nchini kwenda Dubai katika falme za nchi za kiarabu (UAE) kwa ajili ya maonesho matatu tofauti nchini humo. 
 Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella, alisema kuwa wanamuziki hao pamoja na Ommy Dimpoz, wataondoka majira ya saa 8  mchana na kurejea siku ya Jumatato mara tu baada ya maonesho hayo. 

 Alisema kuwa siku ya Ijumaa ambayo itakuwa machi 27, litaanza onesho la kwanza, wakati Jumamosi watafanya onesho la pili na la tatu litafanyika Jumapili. 

 Fella, alisema mwaliko huo maalum ni pamoja na mwanamuziki huyo  wa kizazi kipya, ambaye amesema kuwa atafanya maonesho ya pamoja na YAmoto Band. 
 "Ni mwaliko maalumu wa vijana wangu wa Yamato, pamoja na Ommy Dimpoz. Kwa jinsi tulivyojipanga ninaamini watato burudani nzuri, na kuacha gumzo katika maonesho yote matatu watakayofanya"alisema Fella. 
Yamato ambao hivi karibuni walikuwa nchini Uingereza kwa kufanya ziara ya mwezi mzima na kutoa burudani katika miji tofauti nchini humo, na kujizolea sifa kutokana na uwezo wao wa kufanya onesho live na bendi
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Yaani nyie vijana wa Yamoto, jitahidini sana kuishi hivyo hivyo, msidanganyike na mali za watu na mkasambalatika. Mungu adumishe umoja wenu. Watanzania tunawapenda sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...