BENDI ya muziki wa kizazi kipya ya Yamoto Band na Mwanamuziki wa Kizazi
Kipya Omary Nyebo 'Ommy Dimpoz', kesho wanatarajiwa kuondoka nchini kwenda Dubai katika falme za nchi za kiarabu (UAE) kwa
ajili ya maonesho matatu tofauti nchini humo.
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella, alisema kuwa wanamuziki hao
pamoja na Ommy Dimpoz, wataondoka majira ya saa 8 mchana na kurejea siku ya
Jumatato mara tu baada ya maonesho hayo.

Alisema kuwa siku ya Ijumaa ambayo itakuwa machi 27, litaanza onesho la
kwanza, wakati Jumamosi watafanya onesho la pili na la tatu litafanyika Jumapili.
Fella, alisema mwaliko huo maalum ni pamoja na mwanamuziki huyo wa kizazi
kipya, ambaye amesema kuwa atafanya maonesho ya pamoja na YAmoto Band.
"Ni mwaliko maalumu wa vijana wangu wa Yamato, pamoja na Ommy Dimpoz. Kwa jinsi tulivyojipanga ninaamini watato burudani nzuri, na kuacha gumzo katika maonesho yote matatu
watakayofanya"alisema Fella.
Yamato ambao hivi karibuni walikuwa nchini Uingereza kwa kufanya ziara ya
mwezi mzima na kutoa burudani katika miji tofauti nchini humo, na kujizolea sifa kutokana na uwezo wao wa kufanya onesho live na bendi
.
Yaani nyie vijana wa Yamoto, jitahidini sana kuishi hivyo hivyo, msidanganyike na mali za watu na mkasambalatika. Mungu adumishe umoja wenu. Watanzania tunawapenda sana.
ReplyDelete