Jumla ya kaya masikini elfu Tisa 277 zimetambuliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, katika utekelezaji wa hatua ya awali ya kuzibaini kaya masikini kwenye vijiji na mitaa ikiwa ni mpango wa awamu ya tatu wakuzinusuru kaya masikini unaoratibiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini Tasaf kuputia Halmashauri hiyo.

Taarifa ya Ofisi ya habari na Mawasiliano ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari, imetanabaisha kuwa, wawezeshaji wapatao 72 walijengewa uwezo wa kubaini vigezo kwa kaya masikini, ambapo hojaji zilifanyiaka na jumla ya vijiji 82 na mitaa 12 walifanya dodoso na kuzibaini kaya masikini elfu tisa 277.

Taarifa  hiyo imeeendele kubainisha kuwa, tayari kaya hizo zimepelekwa Tasaf makao makuu ili kufanyiwa uchambuzi wa mwisho unaozingatia vigezo kwa njia ya teknolojia ya kompyuta na mara baada ya kurejea kwa kaya teule, zoezi litakalofuata ilitakuwa ni uandikishaji  kabla ya kuziwezesha kifedha, ambapo kila kaya inatarajia kupata shilingi elfu 38 na 100 kila mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Pamoja na uwezeshaji huo katika ngazi ya kaya, mpango huo pia unakusudia kuibua na kutekeleza miradi ya msingi ya huduma za kijamii kwenye  sekta za Afya, Elimu na Maji katika maeneo ambayo kaya hizo zimetambuliwa.

Aidha, masharti makuu kwa kaya zitakazo teuliwa na kupatiwa fedha kwa kipindi chote cha miaka mitatu ya mradi zitalazimika kuzizalisha kwa kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa au kuanzisha biashara ya kujiingizia kipato huku wale watakaoshindwa kutekeleza masharti hayo wataondolewa.

Katika hatua nyingine timu ya maofisa iliyokuwa ikiendesha zoezi la hojaji ya kuzitambua kaya hizo lilikabilina na changamoto kadhaa ikiwa ni pamaoja na uwelewa mdogo kuwa fedha hizo ni za bure, kuzihusisha Fedha hizo na Asasi maalufu ya(Free Mason) baadhi ya kaya kupatikana maeneo yasiyofikika kwa urahisi asanjari na baadhi ya wananchi kukana kwamba wao si masikini licha ya kutanjwa na wakazi wenzao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...