Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro Kulinjirwa akiongea na
Maafisa Vijana,Waratibu wa Ukimwi na Vijana (Hawapo Pichani) kutoka katika
Mikoa ya Simiyu,Shinyanga na Mwanza alipokuwa akizindua rasmi warsha
kuhusu Stadi za Maisha kwa washiriki hao leo jijini Mwanza ikishirikisha wizara
ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania
.Warsha iyo ya siku nne inafanyika katika hoteli ya Midland. Kushoto kwake
ni Mratibu wa Vijana kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi,Grace
Kessy na wa kwanza kulia ni Mtaalamu wa Stadi za Maisha Bw.Robert
Semkiwa.
Washiriki mbalimbali wa warsha kuhusu Stadi za Maisha
wakimskiliza kwa makini Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro
Kulinjirwa(hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao leo jijini
Mwanza.Bw Kulinjirwa aliwasisitiza washiriki hao kutumia vyema mafunzo
watakayopata ili kubadili maisha yao na ya jamii nzima kwani Stadi za Maisha
ndio kinga dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Mtaalamu
wa Stadi za Maisha Bw.Robert Semkiwa(Aliyesimama) akifurahia jambo na washiriki
wa warsha ya siku nne kuhusu Stadi za Maisha kutoka katika mikoa ya
Mwanza,Simiyu na Shinyanga leo hii jijini Mwanza.Warsha hiyo imeanza leo
ikiwashirikisha Waratibu wa Ukimwi,Maafisa Vijana na Wadau Mbalimbali.Warsha
hii inafanyika katika hoteli ya Midland jijini Mwanza.
Waratibu
wa Ukimwi,Maafisa Vijana na Vijana wakiwa katika Picha ya pamoja na Kaimu
Katibu tawala Mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro Kulinjirwa(aliyekaa mwenye suti ya
khaki),Mtaalamu wa Stadi za maisha Bw.Robert Semkiwa(wa Kwanza kushoto
aliyekaa),Bi Grace Kessy kutoka Tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (wa
pili kutoka kulia waliokaa) na Bw, Godfrey Masawe ambaye ni Afisa Vijana kutoka
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo(wa kwanza kutoka kulia waliokaa).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...