Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama barabarani.

Hali ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna basi hata moja lililoondoka huku daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.

Uongozi wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili kulizungumzia swala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni, kwani wao wanadai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka.
Mabasi ya Abiria yaendayo Mikoani yakiwa yameegeshwa tu kwenye maeneo yake katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar.
Wakina mama hawa wakiwa wamemshikilia Mgonjwa wao waliekuwa wakimsafirisha kwente mkoani, wakiondoka stendi ya kuu ya Mabasi Ubungo baada kukosa usafiri kutokana na mgomo wa vyombo hiyo leo.
Huku Ubungo mambo yako namna hii, ni mwendo wa kupiga mguu tu.
Mijadala ikiendelea kwa wadau mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika kituo kikubwa cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar.
Mara lori likazuiliwa na watu hawa, wakidai kuwa amepakia abiria hivyo anatakuwa kuwashusha kama anataka kuendelea na safari yake.

KUONA PICHA ZAIDI 
BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tusibembelezane. Maisha ya watanzania ni muhimu kuliko utashi wa madereva na wamiliki wa hivyo vyombo. Kama hawataki wafungiwe na leseni zao zifutwe. hatuwezi kuendelea kupoteza maisha yetu na ya ndugu zetu eti kwasababu madereva wanaishinikiza serikali kwa mgomo. Kamanda Mpinga na IGP Mangu uzi ni ule ule. Kwenye Usalama wa Raia hakuna siasi ni sheria tu. Na mkifanikisha hilo mtaweka misingi mizuri na kuponya maisha ya watanzania wengi. Kwenye hilo tusipapase macho wala kumung'unya maneno. Na wandungu Serikalini msiogope eti kwakuwa ni mwaka wa uchaguzi tuwaache waendeleze uzembe wao wakati tutaendelea kupoteza maisha ya watanzania. Tukaze buti na ikibidi wakigoma piga tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...