Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetuma salama za rambirambi kwa familia za washabiki wa timu ya Simba waliopoteza maisha katika ajali ya gari jana mkoani Morogoro wakiwa safarini kuelekea mkoani Shinyanga kuishangilia timu yao dhidi ya Kagera Sugar.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Matina Nkurlu katika taarifa yake aliyoitoa kwa niaba ya kampuni amesema kuwa msiba huu ni mzito kwa watanzania na wapenzi wa soka kwa ujumla.

“Vodacom Tanzania kama mdhamini Mkuu wa ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania bara tumeguswa sana na msiba huu na tunatoa pole kwa familia zilizopoteza jamaa zao katika ajali hii na tunawaombea moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,vilevile tunatoa pole kwa majeruhi wote wa ajali hii na tunawaombea wapone haraka na kurejea katika hali zao za kawaida”.Alisema.

Ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Mkundi katika manispaa ya Morogoro juzi imesababisha vifo vya watu saba na wengine zaidi ya 18 kujeruhiwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro.Leonard Paul amekaririwa akisema kuwa chanjo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva aliyekuwa analiendesha gari hilo.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akiongea na waandishi wa habari( hawapo pichani) wakati alipokuwa akituma salama za rambirambi kwa niaba ya kampuni kwa familia za mashabiki wa timu ya Simba waliopoteza maisha yao kwa ajali ya gari jana Mkoani Morogoro wakiwa safarini kuelekea mkoani Shinyanga kuishangilia timu yao dhidi ya Kagera Sugar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...