Dar es Salaam, 13 April 2015 Finali ya shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika lililoshirikisha washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika chini ya majaji mahiri akiwemo  Akon, Devyne Stephens na Lynnsha  mwisho mwa wiki hii watashirikiana kumtanga rasmi mshindi wa Airtel Trace Afrika.
Airtel kupitia taarifa yake iliyotumwa na ofisa uhusiano wake Jane Matinde imesema “Shughuli nzima ya kumtangaza mshindi itaonyeshwa  kupitia chanel ya Trace inayopatikana katika kituo cha DSTV #325  siku ya jumamosi tarehe 18 April 2015

Shindano hilo kabambe la  Airtel Trace music star lilihusisha washiriki wengi  walioshiriki kupitia kupiga simu na kurekodi mojakwa moja ambapo jumla ya simu zaidi ya milioni mbili na laki tatu  za washiriki wote zilipigwa na kufanya namba ya washiriki wa shindano hili kubwa Afrika kuweza kuzidi mashindano ya Ulaya na marekani kama vile ya voice na idols.

Washiriki 13 kutoka nchi za Afrika waliingia katika kinyanganyiro cha kutafuta mshindi tarehe 28 machi 2015.  Usikose kushuhudia shindano hilo la  kusisimua lenye vionjo vya kila aina, mbwembwe na bashasha tele.

Finali hizi za Airtel Trace Stars zitaonyeshwa siku ya Jumamosi ambapo watazamaji na majaji  watachagua na kutangaza mshindi ambaye atapata dili la kurekodi , kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa mwanamuziki nguli wa nchini Marekani lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500,000/=

Progam hii ya finali itarushwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18 April kuanzia saa tatu Usiku na kurudia siku ya Jumapili tarehe 19 Aprili kuanzia saa kumi jioni katika chaneli ya Trace urban.  Kipindi kitadumu kwa muda wa dakika tisini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...