Meneja
Uragibishi na Mawasiliano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu
Philomena Marijani (aliyesimama)akitoa maelezo mafupi kuhusu semina ya siku 5
kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke itayozungumzia uzuiaji
wa mimba za utotoni kwa wanafunzi wa wilaya hiyo. Semina hiyo inafanyika katika
Shule ya Sekondari Kibasila kuanzia tarehe 13 hadi 17.4.2015.
Baadhi ya
wanafunzi na walimu kutoka Shule 11 za Sekondari katika Wilaya ya Temeke
wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Afisa Elimu-Sekondari wa Wilaya ya Temeke
Ndugu Donald Chavila (hayuko pichani) wakati alipokuwa akifungua rasmi semina
ya siku tano inayozungumzia uzuiaji wa mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Wilaya
hiyo tarehe 13.4.2015 kwenye ukumbi wa sherehe wa Kibasila Sekondari.
Afisa Elimu-Sekondari wa Wilaya ya Temeke Bwana Donald Chavila akifungua
rasmi semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Shule za
Sekondari katika Wilaya ya Temeke. Semina hiyo inaendeshwa na Taasisi ya WAMA,
ikishirikiana na Shirika la Engender Health la Marekani na kufadhiliwa na
Shirika la Misaada la Serikali ya Marekani,USAID.
Mwanafunzi
mshiriki wa semina ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule za
sekondari katika Wilaya ya Temeke akiwasilisha majibu ya majadiliano ya kikundi
chao katika siku ya kwanza ya semina hiyo. PICHA NA JOHN LUKUWI.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...