Pichani juu ni mmoja wa majeruhi akisaidiwa na msamaria mwema mara baada ya kupata ajali. 

 Mtu mmoja amefariki dunia huku wengine 25 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria la Jordan lenye usajili wa namba T 650 AQZ lililokuwa likitokea jijini Mwanza kwenda mkoani Arusha na kupinduka leo wilayani Nzega,Tabora.Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
 Baadhi ya Majeruhi mara baada ya ajali hiyo kutokea.
 Baadhi ya Abiria wakiwa nje ya basi la Jordan mara baada ya kupinduka wilayani Nzega mkoani Tabora na kupelekea kifo cha mtu mmoja.
Mmoja wa abiria akifanya mawasiliano baada ya kunusurika kifo basi la Jordan mara baada ya kupinduka wilayani Nzega mkoani Tabora na kupelekea kifo cha mtu mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mimi sitaelewa wala kuelewa juu ya ajali Tanzania. Nafikiri kuna kitu tumemkosea Mungu turudi kwake. Dhambi zinazotendwa Tanzania hazimpendezi Mungu ndio sababu ya haya yote. Turudi kwa Mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete
  2. mazezeta wakiwa wengi kwenye kiti cha dereva abiria msichoke kulia ovyo hata kutoa POLE wengine tumesha choka tukiendelea kufanya hivyo na sisi tutakuwa hayawani.

    nchi imezidi uzembe kila sehemu inahitaji mabadiliko na wenye nchi wakali ajabu wamezowea shida.

    hivi vifo sio kazi ya mungu tuache kumsingizia kila siku wenye lawama bebeni mizigo yenu sasa.

    mdau.

    kilioni{machozi yamekauka}

    ReplyDelete
  3. madhehebu na misikiti tupige makelele, tufunge tusali tumuombe mwenuezi MUNGU atuepushe na ajali hizi jamani, tuzifunge hizi nguvu za giza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...