Na John Gagarini, Bagamoyo
MKOA wa Pwani umefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni nane kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kipindi cha mwaka 2013/2014.

Hayo yalisemwa juzi wilayani Bagamoyo na Ofisa Misitu wa mkoa huo Daniel Isara, wakati wa maadhimisho ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika kwenye eneo la la Gareza la Kigongoni ambapo ilipandwa zaidi ya miti 3,000.

Isara alisema kuwa fedha hizo zimetokana na kukabiliana na uharibifu wa rasilimali misitu na mazingira ambapo doria ziliimarishwa na ukusanyaji wa mapato kufikia kiasi hicho.

Alisema kuwa hadi kufikia mwezi Januari 2014/2015 makusanyo yalifikia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni sita baada ya wakala hao kuongeza watumishi kwenye ngazi za wilaya.

“Mbali ya mafanikio ya ukusanyaji wa mapato hayo ya Serikali pia mkoa umehamasisha na mwamko umekuwa mkubwa na kuongeza uanzishwaji wa vitalu vya miche na upandaji wa miti kwe taasisi za serikali na zisizo za serikali na watu binafsi kutoka miche ya miti milioni 2,253,136 mwaka 2013/2014 na kufikia milioni 2,663,202 mwaka 2014/2015,” alisema Isara.

Aidha alisema kuwa pia wakala imeweza kuwaondoa wavamizi kwenye misitu ya Ruvu Kaskazini, Ruvu Kusini, Kiloka, Kazimzumbwi na wavuvi kwenye Delta ya Rufiji pia kuweka mipaka ya misitu ya hifadhi kiasi cha kilometa 640 katika hekta 10,704.

“Changamoto zinazoikabili rasilimali ya misitu ni pamoja na ongezeko kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam ambalo huongeza mahitaji ya mkaa na kuni hivyo kuongezeka kwa ukataji na ufyekaji wa misitu na mapori,” alisema Isara.

Alibainisha kuwa kuna wafanyabiashara 320 waliosajiliwa kufanyabiashara ya kuvuna mazao ya misitu mkoani Pwani kwa  mwaka 2013/2014 na 336 mwaka 2014/2015 na zaidi ya asilimia 90 wanatoka nje ya mkoa.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani  Evarist Ndikilo ambaye aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema kuwa taasisi zinazotumia kuni kwa wingi kwa ajili ya kupikia na shughuli nyingine zinapaswa kupanda miti kwa wingi.

Ndikilo alisema kuwa zinapaswa kutumia majiko sanifu yanayotumia kuni au mkaa kidogo ili iwe sehemu ya ubunifu wa kupunguza matumizi makubwa ya nishati ya miti.

Aliwataka wananchi kila mtu kupanda miti ili kulinda mazingira pia mamalaka za serikali za mitaa kuomba vibali vya kuajiri watumishi kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa rasilimali misitu na misitu iliyohifadhiwa inatunzwa na kuzuia wavamizi wanaoingiza mifugo, uchimbaji wa mchanga, kilimo na makazi kwenye misitu.

Mkoa wa Pwani una misitu 34 ya hifadhi yenye jumla ya hekta 335,712 iliyohifadhiwa kisheria na hekta milioni 2.2 ya misitu kwenye ardhi huria ambayo hutegemewa na mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kwa ajili ya matumizi ya nishati za magogo, mbao, samani na matumizi mengine.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akipanda mti kuashiria maadhimisho ya upandaji miti kimkoa yaliyofanyika katika eneo la Gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo. (Picha na John Gagarini).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. How does this translated to the development of coast region????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...