Mkuu wa
kitengo cha sheria wa Wakala wa usalama na afya mahali pa kazi(OSHA),Joyce Mwalubungu, akizungumza na wakandalasi
waliohudhuria kwenye warsha iliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala
pa kazi (OSHA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mshauri
mkuu wa ufundi wa ujasiliamali na miradi kwa vijana Jelous Chirove akizungumza
na wakandarasi waliohudhuria kwenye warsha iliyoandaliwa na wakala wa Usalama
na Afya mahala pa kazi (OSHA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.


Na Avila Kakingo,Globu ya
Jamii.
MAKANDARASI wametakiwa kuwajibika
kwa kuwahudumia wafanyakazi wao wakiwa sehemu ya kazi kwa kulinda afya na
usalama wakiwa kazini.
Hayo
yamesemwa na Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Usalama na afya Mahala
Pakazi (OSHA),Akwilina Kayumba wakati wa Warsha ya Wakandarasi
iliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya sehemu ya
kazi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Shirika la Kazi Duniani,
jijini Dar es salaam.
Warsha kwa hiyo imelenga
kuwajengea uwezo wa Makandarasi katika kuelekea kuadhimisha siku ya
usalama na Afya Mahala Pakazi Duniani ya afya Duniani
itakayofanyika Aprili 28 mkoani Dodoma.
Amesema sekta ya ujenzi ina
wafanyakazi wengi hivyo inatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu katika kuepuka ajali
ambazo zinaweza kutokea wakiwa kazini pamoja na magonjwa.
Kayumba amesema katika
maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahala Pakazi Duniani,Wakala
usalama na afya Mahala Pakazi kwa maadhimisho hayo itakuwa siku ya
maombolezo,majeruhi,magonjwa na vifo vya wafanyakazi mahala pakazi.
Amesema kauali mbiu ya
maadhimisho ya siku usalama na Afya Mahala Pakazi Duniani mwaka huu
ikiwa na kauli mbiu ‘Tushirikiane sote kudumisha usalama na afya sehemu ya
kazi’.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...