Kiongozi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) katika Makazi ya Mishamo, Adolph Bishanga akimkabidhi chandarua na shuka raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses (kulia) baada ya kujifungua mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na UNHCR kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti.
Mkuu wa Makazi ya Ulyakulu, Abdulkarim Mnacho (kushoto) akimpongeza raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses baada ya kujifungua mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wakimbizi wanapewa uraia lakini wa tanzania wanaoishi nje na kuwa raia wa nchi hizo wananyimwa haki ya kuwa raia

    ReplyDelete
  2. Heri mimi manenge sijasema....asia na wapopo wanaochukua pasi kiulani na kutanua nazo ulaya....tunabaki midomo wazi mtu hajui lolote kuhusu Tz lakini ana pasi.

    ReplyDelete
  3. The mdudu, nyie mwageni tu huo uraia kama mpunga lakini huko mbeleni mtakuja kujuta hivi O..kimbunga haikua mikoa yote? Hao kwao kushatulia na hakuna tatizo lolote sasa huo uraia niaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...