Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.



MAFURIKO,Mafuriko,Mafuriko .! Jiji la Dar limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha wengine kukosa makazi.



Maeneo yaliyokumbwa kwa mafuriko ni Mnyamani (Ilala),Bonde la Mpunga (Kinondoni) ,Kigogo (Kinondoni),Mikocheni ( Kinondoni),Vingunguti (Ilala) Tabata Kisiwani (Ilala)na Kurasini (Temeke) na maeneo mengine ambayo hayajawahi kupata mafuriko yamefika.



Mvua hizo zimeharibu miundombinu katika barabara ya Morogoro kwa kujaa maji na kufanya kutokuwepo kwa usafiri kuelekea katikati ya jiji la Dar es Salaam.



Wilaya ya Kinondoni ndio inaongoza kwa maeneo mengi kukumbwa na mafuriko kutokana na watu kujenga katika mikondo ya maji na baadhi ya watu kujenga nyumba katika miundombinu ya maji mitalo ya  maji taka na  kufanya maeneo mengine kutapakaa maji na kuleta adha ya usafiri.



Kwa Wilaya Ilala ni eneo moja ndilo limekuwa likisababisha mafuriko, ni kwa wale waliojenga karibu na bonde la mto Msimbazi  ndio wamekuwa waathirika wa mafuriko kila mwaka.



Wananchi wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hawana msaada wowote huku mvua ikiendelea kunyesha kuanzia majira ya saa 10 jioni na kuamkia leo hadi katika muda huu mvua inatikisa.


Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick amesema kuwa serikali msaada wake ni wale waliopata madhara kutokana na mvua hizo na sio kuwapa makazi na chakula kutokana na kukataa kuhama maeneo hayo na kuishia kuipeleka serikali mahakamani.



Mkuu wa Mkoa amesema serikali ilitoa maeneo mbadala ya kwenda kujenga na kuishi kwa watu wa maeneo ambayo mara kwa mara wamekuwa wakipata mafuriko, walikataa na kuipeleka serikali mahakamani hivyo sasa haiwezi kuwasaidia.


“Sasa sisi tufanye nini tutawaombea sala,lakini msaada kwetu ni wale waliopata madhara ya kiafya kwa ajili matibabu,Serikali ndio itafanya hivyo”amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.



Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema katika mvua zinazoendelea mtu mmoja amepoteza maisha kwa kuanguka katika mto ng’ombe uliyopo eneo la Mburahati jijini Dar es Salaam.



Kamanda Kova amesema aliyepoteza maisha ni Shaban Idd (73) Mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam na mwili wake umeopolewa na kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema amesema ,daraja wa mwanatopa limekatika na kufanya mawasiliano kati ya Kijichi na Mbagala kukosekana.

Katika mvua hizo,wilaya ya Temeke Mtoto mmoja ambaye jina lake halijaweza kupatikana alipoteza maisha kutokana na kuchuliwa na maji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2015

    miaka 50 ya uhuru na bado miundo mbinu ni jambo adimu mno tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2015

    Tunavuna matokeo ya kuwa na mipango miji ya kiholela na kutokuwa na njia za kupitisha maji ya mvua.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2015

    Halafu bado mnasema tulio nje turudi bongo kuna maendeleo sana???dah kwa hali hii bongo should be declared unfit for human settlement!

    mdau
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2015

    ha ha ha ha hiyo picha ya watu wazima wamebebwa mgongoni kama vichanga!! kweli bongo tambarare hahaha

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2015

    Hahahahaha juzi meya wetu wa jiji kashinda afrika nzima......wale waliotoa zawadi kwa hali hii wanaweza kughairi .......

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2015

    Yule meya aliyeshinda afrika anatokea jiji hili sio???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...