Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.
MAFURIKO,Mafuriko,Mafuriko .! Jiji
la Dar limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na
kusababisha wengine kukosa makazi.
Maeneo yaliyokumbwa kwa mafuriko ni Mnyamani
(Ilala),Bonde la Mpunga (Kinondoni) ,Kigogo (Kinondoni),Mikocheni (
Kinondoni),Vingunguti (Ilala) Tabata Kisiwani (Ilala)na Kurasini
(Temeke) na maeneo mengine ambayo hayajawahi kupata mafuriko yamefika.
Mvua hizo zimeharibu miundombinu katika
barabara ya Morogoro kwa kujaa maji na kufanya kutokuwepo kwa usafiri kuelekea katikati ya
jiji la Dar es Salaam.
Wilaya ya Kinondoni ndio inaongoza kwa maeneo
mengi kukumbwa na mafuriko kutokana na watu kujenga katika mikondo ya maji na
baadhi ya watu kujenga nyumba katika miundombinu ya maji mitalo ya maji
taka na kufanya maeneo mengine kutapakaa maji na kuleta adha ya usafiri.
Kwa Wilaya Ilala ni eneo moja ndilo limekuwa
likisababisha mafuriko, ni kwa wale waliojenga karibu na bonde la mto
Msimbazi ndio wamekuwa waathirika wa mafuriko kila mwaka.
Wananchi wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko
hawana msaada wowote huku mvua ikiendelea kunyesha kuanzia majira ya saa 10
jioni na kuamkia leo hadi katika muda huu mvua inatikisa.
Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii,Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick amesema kuwa serikali msaada wake ni
wale waliopata madhara kutokana na mvua hizo na sio kuwapa makazi na chakula
kutokana na kukataa kuhama maeneo hayo na kuishia kuipeleka serikali
mahakamani.
Mkuu wa Mkoa amesema serikali ilitoa maeneo
mbadala ya kwenda kujenga na kuishi kwa watu wa maeneo ambayo mara kwa mara
wamekuwa wakipata mafuriko, walikataa na kuipeleka serikali mahakamani hivyo
sasa haiwezi kuwasaidia.
“Sasa sisi tufanye nini tutawaombea sala,lakini msaada kwetu ni wale waliopata madhara ya kiafya kwa ajili
matibabu,Serikali ndio itafanya hivyo”amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum
ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema katika
mvua zinazoendelea mtu mmoja amepoteza maisha kwa kuanguka katika mto ng’ombe uliyopo eneo la Mburahati jijini Dar es Salaam.
Kamanda Kova amesema aliyepoteza maisha ni
Shaban Idd (73) Mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam na mwili wake umeopolewa
na kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema amesema ,daraja wa mwanatopa limekatika na kufanya mawasiliano kati ya Kijichi na Mbagala kukosekana.
Katika mvua hizo,wilaya ya Temeke Mtoto mmoja ambaye jina lake halijaweza kupatikana alipoteza maisha kutokana na kuchuliwa na maji.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema amesema ,daraja wa mwanatopa limekatika na kufanya mawasiliano kati ya Kijichi na Mbagala kukosekana.
Katika mvua hizo,wilaya ya Temeke Mtoto mmoja ambaye jina lake halijaweza kupatikana alipoteza maisha kutokana na kuchuliwa na maji.

miaka 50 ya uhuru na bado miundo mbinu ni jambo adimu mno tanzania.
ReplyDeleteTunavuna matokeo ya kuwa na mipango miji ya kiholela na kutokuwa na njia za kupitisha maji ya mvua.
ReplyDeleteHalafu bado mnasema tulio nje turudi bongo kuna maendeleo sana???dah kwa hali hii bongo should be declared unfit for human settlement!
ReplyDeletemdau
Ughaibuni
ha ha ha ha hiyo picha ya watu wazima wamebebwa mgongoni kama vichanga!! kweli bongo tambarare hahaha
ReplyDeleteHahahahaha juzi meya wetu wa jiji kashinda afrika nzima......wale waliotoa zawadi kwa hali hii wanaweza kughairi .......
ReplyDeleteYule meya aliyeshinda afrika anatokea jiji hili sio???
ReplyDelete