Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Kampuni ya Majisafi na Majitaka  Dar es Salaam(Dawasco)imeanza rasmi  operesheni kuwakamata watu waliojiunganishia maji kwa njia haramu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema operesheni hiyo itafanyika kanda zote za jiji la Dar es Salaam ikiwa ni kutaka jamii kuacha tabia hiyo.

Amesema kuwa wizi wa maji unafanya watu ambao ndio wateja wa Dawasco kukosa maji na kupata watu wasio wateja wakiwa wameunganisha maji kwa kiwango kikubwa.

“Hatuwezi kuacha maji yawe yanaibiwa huku wateja wetu wanaolipia ankara zao wakikosa, ni lazima hatua zichukuliwe kwa wale wote watakaobainika na wizi wa maji yetu”amesema Luhemeja.

Luhemeja amesema kwa wale watakaotoa taarifa za mtu anayeibia Dawasco  atapewa  Sh.500,000 ambapo kufanya hivyo watamlinda dhidi ya huyo mwizi wa maji.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi,Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na operesheni ya wizi wa maji jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi,Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa operesheni ya wizi wa maji jijini Dar es Salaam.Picha Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2015

    Mheshimiwa Cyprian Luhemeja umekuja na mpango mzuri.

    Tunaomba pia ututazame wenye shida nyingine ya maji.

    Wakazi wa Tabata eneo la ubayaubaya kwa Jijo, tuliunganishiwa mambomba ya wachina mwaka 2008, tangu wakati huo hadi leo maji hayajawahi kutoka hata siku moja.

    Tumewahi kufuatilia katika ofisi za Tabata mara nyingi sana wametueleza wanafahamu tatizo hilo litashughulikiwa sasa huu mwaka wa saba jamani wameshindwa kutusaidia? Tulianza kuomba mmoja mmoja hadi kwa vikundi bila mafanikio.

    Kuna baadhi yetu tuliomba kuunganishiwa maji na tukalipa malipo yote, mimi binafsi nililipa shilingi laki sita mwaka 2008 mwanzoni baadaye wakasema hawawezi kuniunganishia maji kwa sababu yatakuja ya mradi wa wachina na kweli walikuja wakatufungia wengi tu. Nilipofuatilia zaidi zile shilingi laki sita zinaingizwa kwenye bili wakanieleza nitakatwa mpaka zitakapokwisha. Sasa sijui nitakatwa lini maana hayo mambomba ya wachina hayajawahi kutoa maji hata yalipofungwa siku ya kwanza hayakudondosha hata tone moja la maji hadi leo.

    Wote tuliounganishwa tumekuwa tukinunua maji kabla ya mwaka 2008 hadi leo.

    Kwa heshima na taadhima mheshimiwa tusaidie kuangalia hili kwa kushirikiana na ofisi ya tabata wanayodai wanalifahamu tatizo. Jamani mtu akifahamu tatizo si anatakiwa kutafuta suluhisho?

    Asante

    Nawasilisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...