
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Songea Prof. Nomarn Sigalla King akisalimiana na wachezaji wa timu ya jeshi kutoka Mtwara.
Na Amon
Mtega ,SONGEA
MICHEZO ya
majeshi inayoshirikisha vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama briged ya kanda
ya kusini imefunguliwa rasmi na kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu
wa wilaya ya Songea ,Pr Noman sigaa King huku benki ya NMB tawi la Songea
likiwa limetoa msaada wa jezi za mpira wa miguu seti saba ambazo zenye thamani
ya shilingi 3,000,000.
Akiongea
kwenye ufunguzi huo uliyofanyika leo katika uwanja wa michezo wa
majimaji uliyopo Songea ,Sigara alisema kuwa
michezo hiyo itaimarisha mahusiano ya kiulinzi baina ya mipaka yetu ya
Tanzania kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vitakuwa na ushirikiano.
Alisema kuwa
ulinzi wa Tanzania katika mipaka yetu
hautegemei jeshi moja tuu bali ni ushirikiano wa vikosi vya majeshi
mbalimbali kama vikosi hivi ambavyo vimeshirikishwa kwenye michezo hii
iliyozinduliwa na ambayo itarajiwa kufanyika kwa wiki mbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...