Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,ambapo wilaya ya Kisarawe inatarajia kuuza viwanja zaidi ya 291 kwa wewekezaji wa viwand.
wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,ambapo wilaya ya Kisarawe inatarajia kuuza viwanja zaidi ya 291 kwa wewekezaji wa viwand.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa kazini
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali sambamba na Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakimsikiliza Mwenyekiti wa
Halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe, Adamu Ng’imba alipokuwa akifafanua namna ya mji wa Kisarawe utakavyojengwa,kwenye mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakisoma vipeperushi vinavyoeleza namna ya mji wa kisarawe utakavyojengwa.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya
Wilaya ya Kisarawe imetangaza viwanja 291 vilivyopimwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda katika
Wilaya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo, Adamu Ng’imba amesema Halmashauri ya Kisarawe ina mazingira rafiki
kwa uwekezaji wa viwanda kutokana na maeneo hayo yalivyopimwa.
Ng’imba amesema kuwa mradi wa viwanja hivyo umeshirikisha
wananchi wa maeneo hayo ili kuweza kuondokana na migogoro baina ya wawekezaji
na wananchi ili kuepuka malengo yaliyokusudiwa yasifanikiwe.
Amesema katika viwanja vilivyopo katika mradi wa viwanda
asilimia 63 ya fedha zitazopatikana katika uuzaji wa kiwanja zitakwenda kwa
mwananchi ni katika kuepuka migogoro hiyo. Amesema wawekezaji baada ya kukamilisha taratibu zote za
umiliki wa ardhi ni miaka mitatu kama ameshindwa kuendeleza Halmashauri
itachukua na kuuza kwa mtu mwingine.
Ng’imba amesema katika kuondokana na migogoro na ujenzi
holela,Halmashauri imeamua kushirikisha wananchi katika maeneo husika. Amesema watakaopata maeneo ya uwekezaji katika Halmshauri ya
Kisarawe watapata hati ndani ya siku saba na wananchi ndiyo watakaonufaika na
mradi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...