Na Abou Shatry Washington DC
Watanzania walioko nchini Marekani, wamechangisha zaidi ya Dola 3,550 kwa ajili ya kumsaidia ndugu Moh'd Said Moh'd anayehitaji kwenda nchini India kwa matibabu.
Bi Moza Moh'd Khamis akitoa maelezo machache, Maryam Shaaban kulia, pamoja na Bi Asha Haris, Picha zote na (swahilivilla.blogspot.com)
Akifungua shughuli hiyo iliyofanyika May 17, katika Jimbo la Meryland nchini Marekani na kuzijumuisha jumuiya mbali mbali za Kitanzania, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari nchini humo (ZADIA) Bwana Omar Haji Ali, alisema kwamba mkusanyiko huo ni kielelezo cha umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Katika maelzo yake ya ufunguzi yaliyokamilishwa na dua, Bwana Omar alisisitiza kuwa harambee hiyo iliyofanykika nchini Marekani kwa ajili ya kumsaidia kijana aliyeko Zanzibar, ni uthibitisho kuwa jumuiya za Kitanzania nchini humo zina azma ya kuchangia kidhati katika ustawi wa Tanzania na watu wake.
Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) ndugu Omar Haji Ally akifungua harambee kwa dua.
Hongereni na endeleeni na moyo wa kusaidia ambao wanahitaji msaada kama huyo kijana.
ReplyDeleteHiyo ni sadaka njema na Inshallah Mwenyezi Mungu atawaongezea kwenye fungu la wema.