Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

ALIYEKUWA Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk.  Augustine Mahiga ametangaza nia ya kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es salaam leo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mahiga amesema maadili yamemomonyoka na kufanya kuwepo kwa rushwa na ufisadi.

Mahiga amesema ubadhirifu na ufisadi katika taifa kunahitajika kuwepo kwa mwelekeo katika kuweza kupambana na vitu hivyo ili maendeleo yapatikane kwa wananchi.

“Nikipata nafasi hii nitatumikia watu katika kuujenga uchumi imara kwa kila mwananchi kutokana na kuwepo kwa dira na kuondoa matabaka yanayotokana na ubadhirifu wa mali za umma”amesema Mahiga.

Amesema CCM itoe fursa, isifikie utawala wa watu wenye pesa hiyo sio dhamira ya CCM, na watu wanaotoa msaada uwe na kikomo chake.

Mahiga amesema katika kuweza kufikia uchumi wa kati kunatakiwa kupambana na rushwa na ufisadi, bila kufanya hivyo uchumi huo hautafikiwa.
Aliyekuwa Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Augustine Mahiga akizungumza wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari na wananchi wakimsikiliza Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk Augustine Mahiga wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2015

    Hii foleni ya uraisi ni ndefu na inazidi kuongezeka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2015

    Wacha waongezeke kama na wewe umelipia kadi na umejiangalia ukaona unatosha kuongoza watanzania zaidi ya milioni 45 tangaza nia tukisikie halafu kachukue fomu kabla muda haujaisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...