Bayport yasogeza mbele ofa ya viwanja vya mikopo Vikuruti
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI
ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya
mikopo imesogeza mbele huduma yao mpya ya mikopo ya viwanja vilivyopo
Vikukuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa ajili ya kutoa fursa zaidi
ya Watanzania kupata viwanja hivyo vilivyopimwa.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial
Services, Ngula Cheyo, kushoto, akizungumza jambo baada ya kutangaza
kusogeza mbele huduma ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, wilayani
Kibaha, mkoani Pwani, ambapo sasa huduma hiyo imepelekwa mbele hadi Juni
30, mwaka huu. Picha na Mpiga Picha wetu.
Awali ofa ya
huduma hiyo ilipangwa kumalizika Juni 10 mwaka huu, lakini sasa
imepelekwa mbele hadi Juni 30, ikiwa ni ongezeko la siku 20 zaidi kama
njia ya kuhakikisha kwamba wale wenye nia hiyo wanafanikisha ndoto zao
za kumiliki viwanja.
Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services,
Thabit Mndeme, kulia akizungumza jambo baada ya kutangaza kusogeza mbele
huduma ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani
Pwani, ambapo sasa huduma hiyo imepelekwa mbele hadi Juni 30, mwaka huu.
Picha na Mpiga Picha wetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...