Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani akivishwa skafu mjini Babati Mkoani Manyara jana wakati alipohitimisha maadhimisho ya wiki ya 18 ya maziwa ambayo kitaifa ilihitimishwa mkoani Manyara.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Elaston Mbwilo na viongozi wengine wakifuatilia hitimisho la maadhimisho ya wiki ya 18 ya maziwa ambayo kitaifa ilihitimishwa jana Mjini Babati na Dk Kamani.
Ofisa masoko na matukio wa kampuni ya ASAS Dairies Ltd inayozalisha bidhaa zinazotokana na maziwa, Jimmy Kiwelu, akiwaonyesha waandishi wa habari medali tatu za dhahabu walizopata baada ya kuwa washindi wa jumla kwa mwaka wa tatu mfululizo kwa wasindikaji wakubwa wa bidhaa zinazotokana na maziwa kwenye wiki ya 18 ya maziwa iliyohitimishwa jana mjini Babati Mkoani Manyara.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani akimsikiliza Ofisa masoko na matukio wa kampuni ya ASAS Dairies ya Mkoani Iringa, Jimmy Kiwelu baada ya kampuni hiyo kupata ushindi wa jumla kwa mwaka wa tatu mfululizo kwenye wiki ya 18 ya maziwa kitaifa iliyohitimishwa jana Mjini Babati Mkoani Manyara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...